Pata taarifa kuu
MSUMBIJI-USALAMA

Waasi zasiopungua 50 wauawa Kaskazini mwa Msumbiji

Maafisa wa usalama nchini Msumbiji, wamewauwa waasi karibu 50 katika siku za hivi karibuni katika eneo la Cabo Delgado Kaskazini mwa nchi hiyo, êneo ambalo limeendelea kukumbwa na machafuko kwa miaka kadhaa sasa.

Mji mkuu wa Msumbiji, Maputo.
Mji mkuu wa Msumbiji, Maputo. Wikimedia
Matangazo ya kibiashara

Tangu mwaka 2017, makundi ya waasi yaliyojuihami kwa silaha, yamekuwa yakitekeleza mashambulizi dhidi ya maafisa wa usalama na kuvamia majengo ya serikali katika êneo hilo.

Hata hivyo, Waziri wa Mambo ya ndani Amade Miquidade anasema makundi hayo yanazidiwa nguvu na hivi karibuni, waasi kariobu 50 waliauwa katika barabara ya kutoka Chinda kwenda Mbau.

Serikali ya Msumbuji imekuwa ikisema makundi hayo yenye mrenho mkalmi wa kiiskamu, yanatekeleza matukio ya kigaidi na lengo ni kuwatisga wananchi na kuwakoseha imani kwa serikali yao.

Wachambuzi wa siasa nchini humo wanasema kuwa utovu wa usalama Kaskazini mwa Msumbiji ni kwa sababu ya kutaka kudhibiti rasilmali, hasa gesi, amabyo rais Filipe Nyusi ameapa kulinda.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.