Pata taarifa kuu
NIGERIA-IMF-CORONA-AFYA-UCHUMI

Coronavirus: IMF kuipa Nigeria Dola billioni 3.4 kuinua uchumi wake

Shirika la Fedha la Kimataifa, IMF, limeidhinisha Dola billioni 3.4 zitakazotumika katika taifa la Nigeria kukabili athari za virusi vya Corona katika uchumi wa taifa hilo.

Eneo lenye watu wengi, moja ya maeneo ya Jimbo la Kano, siku moja kati ya 14 baada ya serikali kutangaza marufuku ya watu kutembea.
Eneo lenye watu wengi, moja ya maeneo ya Jimbo la Kano, siku moja kati ya 14 baada ya serikali kutangaza marufuku ya watu kutembea. RFIHAUSA/Abubakar Isa Dandago
Matangazo ya kibiashara

Ni hatua inayojiri baada ya serikali ya Nigeria kuomba msaada huo kutoka kwa IMF, kutokana na kudorora kwa uchumi wa taifa hilo.

Hivi karibuni watu 150 waliripotiwa kufariki dunia katika jimbo la Kano kwa maradhi yasiojulikana.

Hata hivyo Mkurugenzi wa hospitali ya mafunzo ya udaktari ya Aminu Kano, Isa Abubakar, aliwaambia wanahabari kuwa huenda watu hao walifariki dunia kwa virusi vya Corona kwa kuwa sio jambo la kawaida idadi kubwa ya watu kufariki kwa mkupuo.

Nigeria kama nchi nyingine nyingi barani Afrika immendelea kuathirika katika sekta mbalimbali kutokana na kuzuka kwa ugonjwa wa Covid-19 nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.