Pata taarifa kuu
NIGERIA-MAUAJI-USALAMA

Nigeria: Watu 47 wauawa na 'majambazi' Katsina

Watu arobaini na saba wameuawa katika shambulio la majambazi wenye silaha dhidi ya vijiji kadhaa katika Jimbo la Katsina, Kaskazini-Mashariki mwa Nigeria, ofisi ya rais wa Nigeria na polisi wa eneo hilo wamesema.

Polisi ya Nigeria ikiwaokoa watu kadhaa kutoka mikononi mwa wapiganaji wenye silaha, katika moja ya shule za Jimbo la Katsina.
Polisi ya Nigeria ikiwaokoa watu kadhaa kutoka mikononi mwa wapiganaji wenye silaha, katika moja ya shule za Jimbo la Katsina. AFP
Matangazo ya kibiashara

Mashambulizi hayo, ambayo "yaliendeshwa kwa wakati mmoja" kulingana na polisi wa eneo hilo, yalitokea Jumamosi, shirika la Habari la AFP limeripoti.

Mashambulizi hayo yalitokea katika wilaya za Dutsenma, Danmusa na Safana kulingana na mkuu wa polisi wa eneo hilo.

Watu walio kuwa kwenye pikipiki walifanya "mashambulizi ya kuliyopangwa kwa wakati mmoja" dhidi ya jamii tatu huko Katsina Jumamosi asubuhi, na kuuwa wakaazi 47, msemaji wa polisi wa serikali ya Jimbo la Katsina, Gambo Isah amesema.

Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari, katika taarifa kwa vyombo vya habari, amelaani "mashambulizi ya ujambazi", huku akithibitisha idadi ya watu arobani na saba waliouawa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.