Pata taarifa kuu
BURKINA FASO-HRW-MAUAJI

Human Right Watch yalaani mauaji dhidi ya raia 31 Burkina Faso

Shirika la kimataifa la haki za binadamu la Human Right Watch, HRW, limenyooshea kidole cha lawama vikosi vya usalama vya Burkina Faso kwa mauaji dhidi ya wakazi 31 wa mji wa Djibo, Kaskazini mwa nchi hiyo.

Djibo inapatikana Kaskazini mwa Burkina Faso.
Djibo inapatikana Kaskazini mwa Burkina Faso. RFI
Matangazo ya kibiashara

HRW imesema kuwa waliuawa Aprili 9 mwaka huu baada ya kukamatwa na kisha kuwekwa katika magari ya jeshi.

Tukio hilo lilitokea Aprili 9, kati ya saa 10 asubuhi na 1:30 mchana, kwa mujibu wa Human Rights Watch. Vikosi vya usalama vilizingira mji wa Djibo siku hiyo asubuhi, na kuanza kufanya ukaguzi wa vitambulisho vya kiraia na kuwakamata raia kadhaa katika sekta ya 7, 8 na ya 9 katika jiji hilo, kabla ya kuwaweka katika magari ya jeshi.

Watu waliotoroka makazi yao kufuatia machafuko, ni miongoni mwa watu waliouawa, vimebaini vyanzo kadhaa vilivyonukuliwa na HRW.

Human Right Watch limetoa wito kwa mamlaka nchini Burkina Faso kuanzisha uchunguzi huru na wa haki na kuwachukulia hatua kali waliohusika na mauaji hayo.

Mamlaka inasema kuwa Aprili 10 waziri wa ulinzi aliomba mahakama ya kijeshi kuanzisha uchunguzi kwa madai hayo ya mauaji.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.