Pata taarifa kuu
LIBYA-UNSC-USALAMA

Ramtane Lamamra asitisha kuwania kwenye nafasi ya mjumbe wa UN kwa Libya

Waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Algeria Ramtane Lamamra ametangaza kwamba amesitisha kuwania kwenye nafasi ya mjumbe wa Umoja wa Mataifa kwa Libya.

Ramtane Lamamra, huko Berlin Mei 9, 2017, kama Waziri wa Mambo ya nje wa Algeria.
Ramtane Lamamra, huko Berlin Mei 9, 2017, kama Waziri wa Mambo ya nje wa Algeria. TOBIAS SCHWARZ / AFP
Matangazo ya kibiashara

Baada ya kujiuzulu kwa Ghassan Salamé mwanzoni mwa mwezi Machi, Ramtane Lamamra aliombwa kushikilia wadhifa huo.

Katika taarifa iliyorushwa kwenye vyombo habari vya Algeria, Ramtane Lamamra amebaini kwamba kumekosekana makubaliano kwa kupitisha jina lake.

Katika taarifa, iliyorushwa hewani Alhamisi jioni, Ramtane Lamamra amebaini kwamba kwanza kabisa- Machi 7 mwaka huu - alitoa idhni yake kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu kanuni kwa nafasi ya Mjumbe Maalum wa Umoja wa Mataifa kwa Libya. Tatizo, "mashauriano ambayo Bwana Guterres amekuwa akifanya tangu wakati huo hayakuonekana kuwa na uwezekano wa kufikia makubaliano kwa Baraza la Usalama na wadau wengine. "

Makubaliano ambayo waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Algeria anaona "ni muhimu kwa kukamilisha ujumbe wa amani na maridhiano ya kitaifa nchini Libya.

Ramtane Lamamra ametangaza kwamba hivi karibuni atamtaarifu Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa kuhusu kujiondoa kwa makubaliano yake ya kanuni yaliyotolewa hapo awali.

Ramtane Lamamra, 67, ambaye ni mwanadiplomasia mzoefu, na ambaye pia amekuwa mpatanishi katika migogoro kadhaa katika nchi mbalimbali barani Afrika, ameamua kuachia ngazi.

Akiungwa mkono na idadi kubwa ya wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Ramtane Lamamra alikuwa anapewa nafasi kubwa ya kuchukuwa nafasi hiyo, wiki chache zilizopita.

Kura ya veto iliyowekwa na Marekani kwa uteuzi wake ilisababisha kujiuzulu kwenye nafasi hiyo

Wataalam wanashuku Falme za Kiarabu (UAE), Misiri na Morocco kwa kushinikiza Washington kukataa uteuzi wa mwanadiplomasia huyo kutoka nchi inayopakana na Libya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.