Pata taarifa kuu
GHANA-AJALI

Ghana: Watu 35 wafariki dunia katika ajali ya barabarani

Karibu watu 35, ikiwa ni pamoja na wanawake na watoto, wamefariki dunia na wengine kujeruhiwa vibaya Jumatatu hii katika ajali ya barabarani huko Kintampo, katikati mwa Ghana, maafisa wa serikali na polisi wamesema.

Ikulu ya rais wa Ghana, inayopatikana Accra, mji mkuu wa nchi hiyo.
Ikulu ya rais wa Ghana, inayopatikana Accra, mji mkuu wa nchi hiyo. Flickr creative commons CC-BY-NC 2.0 S Martin
Matangazo ya kibiashara

Mabasi mawili yamegongana kwenye barabara inayotoka Kintampo-kwenda Tamale katika mkoa wa Bono Mashariki, zaidi ya kilomita 400 kutoka mji mkuu wa Accra.

Watu sita bado wapo katika hali mbaya na wengine 27 wameungua vibaya kwa moto, kwa mujibu wa madhahidi.

"Ninaweza kudhibitisha kwamba idadi ya vifo ni 35," Waziri katika jimbo la Bono Mashariki, Kofi Amoakohene ameliambia shirika la Habari la AFP.

"Kulingana na uchunguzi wa awali, dereva wa basi kubwa alijikuta alitupa barabara yake na kugongana na basi ndogo, na baada ya tukio hilo, magari yote mawili yaliwaka moto," Mkuu wa polisi ya barabarani katika eneo la Kintampo, Francis Adjei Brobey, amewaambia waandishi wa habari.

Ajali kama hizi zinatokea mara kwa mara nchini Ghana kutokana na ubovu wa magari na kutofuata sheria za uendeshaji gari.

Kwa wastani, watu sita hufariki dunia barabarani kila siku, kulingana na mamlaka ya uchukuzi na vitu na watu nchini Ghana (MTTD).

Mwezi Februari 2016, watu 70 wafariki dunia na 13 kujeruhiwa katika katika ajali mbaya ya mabasi mawili kugongana katika jiji moja la Kintampo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.