Pata taarifa kuu
UNICEF-MIGODI-DRC-WATOTO

UNICEF: Umasikini unawasukuma wazazi kuwatuma watoto kufanya kazi migodini

Takwimu za Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia watoto UNICEF, katika ripoti yake inaeleza kuwa watoto 40,000 wanaendelea kufanya kazi katika machimbo ya migodi, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Machimbo ya madini Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Machimbo ya madini Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo PHIL MOORE / AFP
Matangazo ya kibiashara

Mkoa wa Haut Uele, Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo unaongoza kwa visa vya watoto kutumiwa katika machimbo hayo ambayo pia makundi ya waasi yakishtumiwa kuendeleza uchimbaji haramu katika Wilaya ya Wacha.

Imebainika kuwa maelfu ya watoto wanatumiwa na waasi wa LRA na Mbororo katika mkoa wa Haut Uele, na madini yanayochimbwa, kusafirishwa nje ya nchi, kwa mujibu kiongozi wa kiraia Jean Sefa.

“Wale waasi wa LRA wanatokea nchini Uganda wanachukua madini na kukimbilia porini,” alisema.

Aidha, UNICEF inasema katika utafiti huo kuwa, umasikini umechangia sana kwa watoto kujihusisha katika kazi hiyo.

Uchimbaji huu umeendelea kusababisha madhara makubwa, ikiwemo kupoteza maisha kwa watu 31 wiki mbili zilizopita katika mgodi wa Ndiyo.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.