Pata taarifa kuu
ZAMBIA-MAREANI-USHIRIKIANO

Marekani yamuita nyumbani balozi wake Zambia baada ya kukemea kufungwa kwa wapenzi wa jinsia

Marekani imemuita nyumbani balozi wake nchini Zambia. Uamuzi ambao unafuatia matamshi ya Rais wa Zambia Edgar Lungu ambaye alitoa uamuzi kwamba mwanadiplomasia huyo wa Marekani hatakiwi kuendelea na kazi yake nchini Zambia.

Rais wa Zambia Edgar Lungu hakufurahishwa na msimamo wa balozi wa Marekani nchini Zambia baada ya kukemea kufungwa kwa wapenzi wa jinsia.
Rais wa Zambia Edgar Lungu hakufurahishwa na msimamo wa balozi wa Marekani nchini Zambia baada ya kukemea kufungwa kwa wapenzi wa jinsia. Β© REUTERS/Rogan Ward
Matangazo ya kibiashara

Balozi Daniel Foote alikosoa vikali hatua ya Zambia ya kuwafunga jela wapenzi wa jinsia moja, vyanzo vya ubalozini vimesema.

Serikali imemshtumu kwa kujaribu kushinikiza sera zitakazo fuatwa na Rais Edgar Lungu.

"Huwezi kulazimisha serikali kufanya maamuzi fulani - 'kwasababu tu munatupa msaada, tunataka nyinyi mufanye hivi' - hilo haliwezekani," Waziri wa Mambo ya Nje wa Zambia Joseph Malanji ameiambia BBC.

Mwezi Novemba, balozi wa Marekani nchini Zambia alisema kuwa ameshtushwa na uamuzi wa jaji wa kuwafunga wanaume hao kifungo cha miaka 15 gerezani baada kupatikana wakifanya mapenzi mwaka 2017.

Katika taarifa iliyotolewa mapema mwezi huu, Bwana Foote amesema alikuwa akionyesha kutoridhishwa kwake na sheria iliyotumika na kifungo kilichotolewa, mtazamo ambao hakukubaliana nao.

Wapenzi hao wa jinsia moja walikuwa wamekodi chumba cha kulala na mfanyakazi mmoja akachungulia kupitia dirisha lililokuwa wazi na kuwafumania wakifanya ngono, mahakama ilifahamishwa hivyo.

Bwana Foote aliongeza kuwa msadaa wa mamilioni ya fedha umefujwa lakini hakuna ambaye ameshtakiwa kwa makosa ya rushwa.

Zambia ni moja ya nchi zinazopokea kiwango kikubwa cha msaada kutoka Marekani takribani dola milioni 500 kwa mwaka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.