Pata taarifa kuu
MALI-SIASA-USALAMA

Rais wa zamani wa Mali Toumani Touré arejea nchini

Rais wa zamani wa Mali Amadou Toumani Touré aliyeondolewa madarakani na jeshi mwaka 2012 baada ya kuongoza nchi hiyo kwa miaka 10 amerejea nyumbani.

Rais wa zamani wa Mali Amadou Toumani Touré alikimbilia uhamishoni nchini Senegal baada ya mapinduzi ya kijeshi mwaka 2012. Alirudi Bamako kwa mara ya kwanza mwaka 2017. Tangu Jumapili, Desemba 15 amerejea nchini Mali.
Rais wa zamani wa Mali Amadou Toumani Touré alikimbilia uhamishoni nchini Senegal baada ya mapinduzi ya kijeshi mwaka 2012. Alirudi Bamako kwa mara ya kwanza mwaka 2017. Tangu Jumapili, Desemba 15 amerejea nchini Mali. MICHELE CATTANI / AFP
Matangazo ya kibiashara

Baada ya kuondolewa madarakani, rais huyo wa zamani alikimbilia nchini Senegal, na baada ya kurejea nyumbani mwishoni mwa wiki iliyopita, alipokelwa na wafuasi wake katika uwanja wa ndege na nje ya nyumbani kwake.

Kiongozi huyo wa zamani ambaye anakumbukwa kwama baba wa demokrasia nchini Mali, licha ya kuondolewa madarkani mwaka 2012 amekuwa akiheshimika kwa kumaliza uongozi wa kijeshi nchini mwake, baada ya kuandaa uchaguzi mwaka 1992 na baadaye kuingia madarakani baada ya miaka 10.

Toure mwenye umri wa miaka 71, amerejea nyumbani wakati taifa hilo la Afrika Magharibi likiendelea kukabiliwa na utovu wa usalama, hasa eneo la Kasakazini ambalo limeeendelea kushuhudia raia na wanajeshi kushambuliwa na wapiganaji wa Kijihadi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.