Pata taarifa kuu
BURKINA FASO-MAUAJI-USALAMA

Burkina Faso: Kanisa la Kiprotestanti lalengwa na shambulio Mashariki mwa nchi

Kanisa la Kiprotestani linaomboleza vifo vya waumini wake 14 waliouawa Jumapili Desemba 2 wakati wa ibada. Kanisa la Kiprotestanti katika mji wa Hantoukoura, mashariki mwa Burkina Faso lilivamiwa na watu waliojihami kwa silaha wasiojulikana.

Askari wa Burkina Faso wakiwa katika mafunzo (Picha ya kumbukumbu).
Askari wa Burkina Faso wakiwa katika mafunzo (Picha ya kumbukumbu). Β© ISSOUF SANOGO / AFP
Matangazo ya kibiashara

Makundi ya kijihadi yameonyeshewa kidole cha lawama kwamba yanaendelea kuhatarisha usalama kwenye sehemu za ibada.

Vitendo vya makundi ya kijihadi kushambuliwa sehemu za ibada vimeongezeka.

Shambulio hilo liliendeshwa na "watu waliojihami kwa silaha za kivita," kwa mujibu wa chanzo cha usalama, kilichonukuliwa na shirika la Habari la AFP. Waumini, ikiwa ni pamoja na mchungaji wa kanisa hilo na watoto, "waliuawa kikatili," chanzo hicho hicho kimebaini.

Katika taarifa yake, ofisi ya gavana imebaini kwamba "vikosi vya ulinzi na usalama" vimetumwa "kutoa msaada kwa watu waliojeruhiwa."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.