Pata taarifa kuu
URUSI-AFRIKA-USHIRIKIANO

Mkutano kati ya Urusi na Afrika waanza Sochi

Mkutano wa kwanza kati ya Urusi na Afrika unafunguliwa leo Jumatano, Oktoba 23 katika mji wa Sochi, mkutano ambao utaangazia kuhusu suala la ushirikiano kati ya nchi za Afrika na Urusi. Lakini Moscow tayari imeweka masilahi yake katika mataifa mengi ya bara la Afrika.

Abdel Fattah al-Sissi (kushoto) ni mmoja washirika muhimu wa Vladimir Putin barani Afrika (picha kumbukumbu).
Abdel Fattah al-Sissi (kushoto) ni mmoja washirika muhimu wa Vladimir Putin barani Afrika (picha kumbukumbu). © REUTERS/Mihail Metzel/RIA Novosti/Kremlin
Matangazo ya kibiashara

Mkutano huo unafanyika chini ya uenyekiti wa rais Vladimir Putin na kiongozi mwenzake wa Misri ambaye pia ni mwenyekiti wa Muungano wa Afrika, Abdel Fattah el-Sisi.

Urusi inafanya biashara muhimu na nchi za Afrika Kaskazini, hasa Misiri na Algeria. Urusi ni nchi ya kwanza inayouza silaha zake barani Afrika kupitia nchi hizi mbili.

Kremlin imeidhinisha uhusiano wa kutosha kiuchumi, kiusalama na kisiasa na Afrika.

Kwa historia, Misri ilikuwa eneo la kimkakati kwa Urusi kuingiza na kuuza silaha zake barani Afrika, kisha nguzo ya sera za Urusi katika nchi za Kiarabu za Afrika kuuazia kwa utawala wa Nasser hadi kuvunjika kwa uhusiano huo mnamo mwaka 1972 chini ya utawala wa Sadat.Nchi hizi mbili zilifufua tena uhusiano wao baada ya kurudi tena utawala wa kijeshi nchini Misri mnamo mwaka 2013.

Urusi pia ilianzisha uhusiano na nchi kadhaa za Afrika wakati wa Vita Baridi, kwa kutaka kutafuta uungwaji wake mkono kwa nchi hizo.

Angola, Madagascar na Ethiopia ni miongoni mwa nchi hizo. Urusi ina uhusiano tosha na Angola. Uhusiano huo umeimarika zaidi baada Rais wa sasa wa nchi hiyo Joao Lourenço aliypata mafunzo jijini Moscow kuchukuwa madaraka ya uongozi wa nchi. Kwa sasa Urusi imejikita katika sekta ya almasi nchini Angola.

Urusi pia imeimarisha uhusiano na Madagascar.

Moscow itajaribu kuimarisha zaidi uhusiano huu wakati wa mkutano wa kwanza baina ya Urusi na Afrika unaofanyika mjini Sochi kuanzia leo tarehe 23 hadi kesho Alhamisi Oktoba 24. Ratiba ya mkutano huo ni kujadili nishati, madini na ushirikiano wa kijeshi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.