Pata taarifa kuu
CHAD-USALAMA

Chad: Idriss Deby atangaza hali ya dharura katika mikoa miwili ya mashariki mwa nchi

Rais wa Chad, Idriss Deby ametangaza hali ya dharura katika mikoa miwili mashariki mwa nchi hiyo. Hali hiyo itadumu miezi mitatu, baada ya mapigano makali kati ya jamii. Mapigano yaliyosababisha vifo vya watu kadhaa mnamo mwei Agosti.

Rais wa Chad Idriss Deby ametangaza hali ya dharura katika mikoa miwili ya Chad kufuatia mapigano kati ya jamii.
Rais wa Chad Idriss Deby ametangaza hali ya dharura katika mikoa miwili ya Chad kufuatia mapigano kati ya jamii. © ludovic MARIN / AFP
Matangazo ya kibiashara

Mikoa hiyo miwili ya Sila na Ouaddai inapatikana kwenye mpaka na Sudani. Migogoro kati ya wakulima na wafugaji wahamaji huwa ikitokea mara kwa mara katika eneo hili. Mapigano makali yaliripotiwa hivi karibuni kati ya jamii hizi baada ya kupatikana kwa miili miwili ya vijana kutoka jamii ya wafugaji.

Katika mapigano hayo watu zaidi ya kumi waliuawa.

Siku kumi zilizopita, katika mkutano na waandishi wa habari, Rais Idriss Déby alibaini kwamba atazuru eneo la tukio. Katika ziara yake siku ya Jumapili katika mji wa Goz-Beida, mji mkuu wa mkoa wa Sila, rais wa Chad aliahidi kutuma jeshi ili kutuliza hali hiyo. "

"Kama kunatokea makabiliano kati ya jamii, polisi inatakiwa kufyatua hewani risasi tatu, na kama hakuna jibu lolote, watu ambao hawatotii kwa hilo watapigwa risasi, " amesema Idriss Déby. Pia amewataka raia wote katika eneo hilo kupokonywa silaha, kwani raia kumiliki silaha ndio chanzo cha mapigano mabaya.

Silaha zinaingia nchini Chad kupitia nchi jirani, kama vile Sudani, lakini pia Libya na Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Rais Deby pia ametoa agizo kwamba kwa miezi mitatu ijayo, hakuna pikipiki yoyote ambayo itafanya kazi katika eneo hilo ambalo ni rahisi kuingia Sudan, kwa nji zisizo kuwa halali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.