Pata taarifa kuu
DRC-UN-USALAMA

Umoja wa Mataifa waongeza muda wa vikwazo kwa baadhi ya watu DRC

Wakati huu ambapo mamia ya raia wanakimbia mapigano ya kikabila mashariki mwa DRC, Umoja wa Mataifa umeongeza muda wa makataa ya silaha, kuzuia mali na zuio la kutosafiri kwa baadhi ya watu nchini humo hadi mwezi Julai mwakani.

Gari ya Umoja wa Mataifa ikipiga doria katika eneo la Djugua, Jimboni Ituri mwezi Machi 2018 (Picha ya kumbukumbu).
Gari ya Umoja wa Mataifa ikipiga doria katika eneo la Djugua, Jimboni Ituri mwezi Machi 2018 (Picha ya kumbukumbu). ALEX MCBRIDE / AFP
Matangazo ya kibiashara

Vikwazo vya umoja wa Mataifa vinazikataza nchi kusambaza au kuyauzia silaha makundi ya waasi nchini DRC, nchi ambayo imeshuhudia hali tete ya usalama tangu miaka ya 1990 na hivi karibuni machafuko kwenye jimbo la Ituri.

Pendekezo lililowasilishwa na Ufaransa lilipitishwa kwa idadi kubwa ya kura za nchi wanachama, ambapo linazitaka nchi kuendelea kuweza vikwazo vya kusafiri kwa viongozi wa waasi na wanasiasa pamoja na kuzuia mali zao.

Kwenye taarifa yake Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linasema machafuko yanayoendelea nchini humo ni tishio kwa usalama wa dunia na ukanda.

Pendekezo hilo pia limeitaka Serikali ya DRC kuharakisha uchunguzi wa mauaji ya wataalamu wake wawili pamoja na raia wanne wa nchi hiyo waliouawa mwezi Machi mwaka 2017.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.