Pata taarifa kuu
DRC-TANZANIA

Rais wa DRC Felix Tshisekedi kufanya ziara ya kwanza Tanzania

Rais mpya wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Felix Tshisekedi Alhamisi ya wiki hii kwa mara ya kwanza tangu achaguliwe kwake atafanya ziara ya siku 2 nchini Tanzania ambapo atakutana kwa mazungumzo na mwenyeji wake rais wa Tanzania John Magufuli. 

Rais wa DRC, Félix Tshisekedi ambaye ataanza ziara ya siku 2 nchini Tanzania, Juni 13, 2019
Rais wa DRC, Félix Tshisekedi ambaye ataanza ziara ya siku 2 nchini Tanzania, Juni 13, 2019 REUTERS/Baz Ratner/File Photo
Matangazo ya kibiashara

Rais Tshisekedi atawasili majira ya saa kumi jioni alasiri ambapo atapokelewa na viongozi mbalimbali wa Serikali ya Tanzania.

Akiwa nchini Tanzania rais Tshisekedi anatarajiwa kutembelea bandari ya Dar es Salaam kabla ya baadae kukutana kwa mazungumzo na mwenyeji wale kwenye ikulu ya magogoni.

Ziara yake ni sehemu ya Kujitambulisha kwa rais Magufuli lakini pia kuendeleza ushirikiano wa kiuchumi, kibiashara na kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili jirani.

Kwa mujibu wa vyanzo kutoka katika ikulu ya Kinshasa, rais Tshisekedi na mwenyeji wake wanatarajiwa kuzungumza kuhusu hali ya biashara baina ya nchi hizo mbili huku DRC ikiwa ni mtumiaji mkubwa wa bandari ya Dar es Salaam kupitishia mizigo yake.

Mbali na hali ya kibiashara viongozi hawa watazungumzia pia masuala ya hali ya usalama nchini DRC na hasa kwenye eneo la Mashariki mwa nchi hiyo ambako Tanzania imetuma wanajeshi wake kusaidia kulinda amani.

Wadadisi wa mambo pia wanaona viongozi hawa watagusia suala la ushirikiano wa kwenye mipaka na hasa kuhusu wakimbizi wa DRC ambao baadhi yao hawajarejea nyumbani.

Mamia ya raia wa DRC wanaishi na kufanya kazi nchini Tanzania, ambapo pia imeripotiwa huenda rais Tshisekedi akakutana nao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.