Pata taarifa kuu
TANZANIA-SADC-SIASA-DIPLOMASIA

Mkutano Wa 39 Wa SADC Kufanyika Tanzania

Tanzania inatarajia Kuwa mwenyeji wa mkutano Wa 39 wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini Mwa Afrika SADC unaotazamiwa kufanyika Mwezi Agosti mwaka huu.

Waziri wa Mambo ya nje wa Tanzania Profesa Palamagamba Kabudi (Katikati) akizungumza na wanahabari jijini Dar es salaam Mei 08 2019
Waziri wa Mambo ya nje wa Tanzania Profesa Palamagamba Kabudi (Katikati) akizungumza na wanahabari jijini Dar es salaam Mei 08 2019 RFI/Fredrick Nwaka
Matangazo ya kibiashara

Mbali Na agenda nyingine za mkutano huo, Tanzania itapokea kijiti cha Uenyekiti Wa SADC Kutoka Kwa Namibia.

Waziri wa mambo ya nje, Ushirikiano Wa Afrika Mashariki, kikanda na Kimataifa Profesa Palamagamba Kabudi amwaambia wanahabari Jijini Dar es Salaam kuwa wajasiriamali wanapaswa kuchangamkia mkutano huo.

"Tutakuwa Na Viongozi Wa Mataifa 16 yanayounda jumuiya ya sadc Na Rais Magufuli atapokea Kiti Cha Uenyekiti Kutoka kwa Rais wa Namibia Hage Geingog. Nawaomba Watanzania wajiandae kwa ugeni mkubwa utakaowasili Nchini,"Amesema Profesa Kabudi.

Mkutano Kama huu ulifanyika Tanzania Mara ya Mwisho mwaka 2003/2004 ambapo rais wakati huo Benjamin Mkapa Alichaguliwa Kuwa Mwenyekiti Wa jumuiya Hiyo.

Joseph Nourrice, Naibu Katibu Mkuu Wa SADC amesema Sekretarieti ya Jumuiya hiyo itashirikiana Na Tanzania Ili Kuhakikisha mkutano huo unafanyika kwa mafanikio.

Katika hatua nyingine Profesa Kabudi amearifu kuwa kabla ya kufanyika kwa mkutano huo, kutakuwa na maonyesho ya viwanda ya SADC yatakayofanyika Jijini Dar es Salaam.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.