Pata taarifa kuu
SUDANI-SIASA-USALAMA-MAANDAMANO

Waandamanaji wasitisha mazungumzo na jeshi Sudani

Kiongozi wa Baraza la kijeshi la Mpito nchini Sudani, Abdel Fattah Burhan, ameonekana kwenye televisheni ya taifa akitangaza kuwa Baraza la Jeshi limejitolea "kukabidhi madaraka kwa raia."

Waandamanaji mbele ya Wizara ya Ulinzi jijini Khartoum tarehe 21 Aprili 2019.
Waandamanaji mbele ya Wizara ya Ulinzi jijini Khartoum tarehe 21 Aprili 2019. REUTERS/Umit Bektasa
Matangazo ya kibiashara

Kwa upande wao, viongozi wa maandamano wamesitisha mazungumzo na jeshi na kutoa wito wa kuzidisha maandamano, kwa mujibu wa mmoja wa wasemaji wa kundi hilo, aliyenukuliwa na shirika la Habari la AFP.

Ni mara ya kwanza Abdel Fattah Burhan kutoa mahojiano tangu Omar al-Bashir kutimuliwa mamlakani tarehe 11 Aprili, na ni mahojiano yake ya kwanza tangu alipochukuwa nafasi ya Jenerali Ibn Auf kwa kuongoza Baraza la kijeshi.

Abdel Fattah Abdelrahman Burhan ametaka kuwahakikishia waandamanaji kwa kile wanachodai. Kwa siku kadhaa waandamanaji wamekuwa wakidai jeshi kukabidhi madaraka kwa raia. Bw Burhan ameahidi kukabidhi madaraka kwa raia. Abdel Fattah Abdelrahman Burhan ameahidi kwamba wiki hii atajibu madai ya waandamanaji.

Wakati huo huo kundi la wasomi, APS, ambalo ni miongoni mwa makundi yaliyoshiriki maandamano na kupinga utawala wa Omar Hassan al-Bashir, limesitisha kutangaza orodha watu wake watakaoshiriki katika serikali ya kiraia.

Mazungumzo yalianza tena Jumamosi, Aprili 20 kati ya jeshi na viongozi wa maandamano. Chama cha wasomi nchini Sudan (APS) kilishiriki mazungumzo hayo katika mstari wa mbele. Chama hiki kiliitisha mkutano na waandishi wa habari jana Jumapili jioni ili kutangaza majina ya wajumbe watakaounda Baraza la kiraia. Kwa uhakika, orodha ya majina ilikuwa imeandaliwa. Lakini Jumapili jioni APS ilitangaza kuachana na mpango huo ikibaini kwamba ahadi za Baraza la Jeshi hazieleweki, na haitoshelezi madai ya waandamanaji na kuamua kusitisha mpango huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.