Pata taarifa kuu
COMORO-UCHAGUZI-SIASA

Upinzani wawasilisha malalamiko yao kwa Tume ya Uchaguzi Comoro

Siku mbili kabla ya kutamatika kwa muda wa kampeni za uchaguzi nchini Comoro, wapinzani dhidi ya rais Azali Asumani nchini humo wamewasilisha malalamiko kwa Tume huru ya Uchaguzi kuhusu wasiwasi walionayo kufuatia kauli zinazotolewa kutoka upande wa utawala, na rais kuvunja sheria ya uchaguzi.

Moroni, mji mkuu wa visiwa vya Comoro.
Moroni, mji mkuu wa visiwa vya Comoro. TONY KARUMBA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo wapinzani hao wanasema kauli zinazotolewa na waziri wa mambo ya ndani katika kipindi hiki hazikubaliki.

“Anajiamini kuwa sheria zaidi ya sheria, hasa kwamba amekuwa akidai katika kampeni za hadhara kwamba yeye ndie atatangaza matokeo ya uchaguzi, na yeye ndie anaeandaa uchaguzi, hivyo tumekuja kukumbusha tume ya uchaguzi kuchukuwa jukumu lake, vinginevyo nasi tutachukuwa jukumu letu” , amesema brahim Abdulrazak Azida, mratibu wa umoja wa vyama vya upinzani.

Upande wake katibu mkuu wa Tume huru ya Uchaguzi, Mzede Afine Saidi amehidi kwamba hii leo tume huru ya uchaguzi CENI itatoa tamko kueleza kwamba tume huru ya Uchguzi na mahakama ya kikatiba ndio taasisi pekee zinazo ruhusiwa kutangaza matokeo.

“Taasisi yoyote itayo toa matokeo yatakuwa ni matokeo batili, sisi ni tume huru, tangu 2014, kuna mambo mengi yamebadilika, tumekwisha simamia uchaguzi mara saba, itakuwa ni hivo, wananchi ndio wataoamuwa” amesema Mzede Afine Saidi.

Licha ya kwamba upinzani hauna mgombea mmoja, unafanya kila jitihada kuungana kulinda mchakato wa uchaguzi wakati huu kampeni zikitarajiwa kutamatika Ijumaa March 22.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.