Pata taarifa kuu
DRC-UN-MONUSCO-USALAMA

Umoja wa Mataifa wajiandaa kuondoa askari wake DRC

Umoja wa Mataifa umeanza kuweka mipango ya kuanza kuwaondoa wanajeshi wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ikiwa ni kubadilisha malengo ya jeshi hilo nchini humo.

Walinda amani wa Monusco kutoka Pakistani wakipiga doria katika mitaa ya Uvira, wilayani Fizi.
Walinda amani wa Monusco kutoka Pakistani wakipiga doria katika mitaa ya Uvira, wilayani Fizi. MONUSCO/Force
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii imebainishwa na Afisa wa Umoja wa Mataifa ambaye hakutaka jina lake kutajwa, ambaye amesema baada ya usalama kuanza kuimarika katika maeneo kadhaa, hali ya kisiasa kubadilika na nchi hiyo kuwa na rais mpya, MONUSCO inafanyiwa mabadiliko taratibu.

Jeshi la Umoja wa Mataifa limekuwa nchini DRC kwa karibu miaka 20, likiwa na wanajeshi wapatao 16,000 lengo likiwa ni kuwalinda raia na kuzuia mashambulizi ya waasi, lakini raia wengi wa DRC hasa kutoka Mashariki mwa nchi hiyo wamekuwa wakisema kwa kiasi kikubwa jeshi hilo halijasaidia.

Iwapo mpango huo, utafanikiwa, huenda katika siku zijazo idadi ya wanajeshi wa MONUSCO itaanza kupunguzwa na hili linakuja wakati huu muda wa kuhudumu kwa jeshi hilo, kwa mujibu wa azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, ukitarajiwa kumalizika hivi karibuni.

Hata hivyo, amesisitiza kuwa ni lazima MONUSCO ishirikiane kikamilifu na serikali ya rais Felix Thisekedi kuhakikisha kuwa mabadiliko hayo yanafanyika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.