Pata taarifa kuu
MISRI-USALAMA-AJALI

Watu 20 wafariki dunia katika kisa cha moto katika kituo cha treni Cairo

Watu ishirini wamefariki dunia na wengine 40 wamejeruhiwa katika kisa cha moto kilichotokea Jumatano (Februari 27) katika kituo cha kati cjijini Cairo, nchini Misri, kwa mujibu wa Waziri wa Afya wa Misri.

Maafisa wa idara ya dharura wakifanya uchunguzi wa kwanza baada ya kisa cha moto katika kituo cha kati cha treni jijini Cairo, Februari 27, 2019.
Maafisa wa idara ya dharura wakifanya uchunguzi wa kwanza baada ya kisa cha moto katika kituo cha kati cha treni jijini Cairo, Februari 27, 2019. © REUTERS/Amr Abdallah Dalsh
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa mwandishi wetu huko Cairo, Alexandre Buccianti tukio hilo limetokea kabla ya saa nne saa za Misri wakati treni ambayo haikuwa na mabehewa ilipokosea barabara yake na kuangukia kwenye jengo nambari sita la kituo cha Kati cha Cairo.

Hali hiyo ilisababiosha kutokea kwa mlipuko wa pipa la treni hiyo linalohifadhi mafuta ya Diesel na kusababisha mgahawa uliokuwa karibu na eneo hilo kuteketea kwa moto.

Hata hivy moto huo ulizimwa haraka. Watu waliofariki duni na majeruhi wamepelekwa katika hospitali jirani. Ajali zhuwa zikitokea mara kwa mara nchini Misri. ajali za treni na mikasa ya moto husababisha maafa mengi kila mwaka nchini Misri.

Mnamo mwezi Februari 2002, zaidi ya watu 300 walifariki dunia baada ya treni waliokuemo kuteketea kwa moto.

Waziri Mkuu Mustafa Madbouli amezuru eneo la tukio na kuahidi kutoa mwanga kuhusu ajali ajali. "Tutaweza kutokubaliana na mtu yeyote aliyehusika na kisa hiki kuhakikisha waathirika wanatendewa haki," `mustafa Madbouli amesema.

Kutokana na ajali hiyo Waziri wa Usafiri Hicham Arafat ameomba kujiuzulu, ombi ambalo Waziri Mkuu amekubali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.