Pata taarifa kuu
AU-SIASA-DRC-MADAGASCAR

Viongozi wa Afrika wakutana jijini Addis Ababa

Viongozi wa Umoja wa Afrika wanakutana kwa siku ya pili katika makao makuu ya Umoja huo jijini Addis Abeba nchini Ethiopia, ambapo ma rais Andy Rajoelina na Felix Tshisekedi wamepokelewa kama ma rais wapya kwenye Umoja huo. Ali Bilali na maelezo zaidi.

Viongozi wa mataifa ya Afrika wakikutana jijini Addis Ababa nchini Ethiopia
Viongozi wa mataifa ya Afrika wakikutana jijini Addis Ababa nchini Ethiopia Cristiana Soares
Matangazo ya kibiashara

Mambo matatu ndio yaliogubikwa kwenye uzinduzi wa mkutano wa viongozi hao kwanza kabisa ilikuwa ni kubadilishana kwa uongozi baina ya rais Paul Kagame wa Rwanda aliemkabidhi uongozi rais wa Misri Abdel Fatah al Sissi, kiongozi anayetafua ushawishi katika mataifa ya Afrika ambae amekuwa akishukiwa kutaka kuzuia mchakato wa kuimarisha ushirikiano ulioanzishwa na rais Paul Kagame.

Hata hivo, Mwenyekiti mpya wa Umoja wa Afrika Abdel Fattah al-Sissi bila kutoa mifano halisi ameahidi kuendeleza mageuzi ya kiuchumi na ya kifedha ya Umoja wa Afrika.

Katika hotuba yake ya kwanza, rais huyo wa Misri alifafanua mambo matatu atayoyapa kipao mbele katika ungozi wake kama mwenyekiti wa umoja wa Afrika:- Kuendeleza miundombinu, kuongeza kasi ya kuingia katika Eneo la Biashara huria la Afrika (CFTA), na kutoa ajira pia kwa vijana wa bara.

Mkutano huo pia ulikuwa fursa ya kumteua mwenyekiti wa Umoja wa Afrika mwaka wa 2020 ambapo itakuwa ni Afrika Kusini, iwapo rais wake Cyril Ramaphosa, atathibitishwa kuwa rais e katika uchaguzi mkuu unaofanyika mwaka huu.

Mkutano huo umeshuhudia pia Uwepo wa Marais wawili wapya waliochaguliwa Andry Rajoelina rais mpya wa Madagascar na Felix Tshisekedi kwa DRC.

Hakuna upinzani wowote ulioshuhudiwa juu ya matokeo ya mgogoro wa uchaguzi nchini DRC, wakuu wa nchi kila mmoja alimshukuru na kumpongeza rais wa Kongo utafkiri hakuna kilichotokea huko Congo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.