Pata taarifa kuu
KENYA-ZANZIBAR

Boti iliyotengenezwa kwa mabaki ya plastiki kufanya safari ya kihistoria

Boti ya asili iliyotengenezwa kwa kutumia mabaki ya plastiki yaliyokuswanya kutoka katika fukwe za Kenya, mwezi ujao inatarajiwa kufanya safari yake ya kwanza ikitokea kwenye mji wa Lamu kuelekea visiwani Zanzibar nchini Tanzania.

Boti iliyotengenezwa kwa kutumia mabaki ya plastic. Picha kwa hisani ya shirika la umoja wa Mataifa linalohusika na Mazingira UNEP
Boti iliyotengenezwa kwa kutumia mabaki ya plastic. Picha kwa hisani ya shirika la umoja wa Mataifa linalohusika na Mazingira UNEP www.unenvironment.org
Matangazo ya kibiashara

Boti hii itasafiri umbali wa kilometa zaidi ya 500 na itasimama katikaka visiwa kadhaa ili kueneza uwelewa kuhusu madhara yanayotokana na matumizi ya plastiki kwa bahari.

Ali Noor Ismael, katibu mkuu wa mazingira nchini Kenya, anasema mazingira ya fukwe nyingi za bahari Afrika yamekuwa yakichafuliwa kwa plastiki, hatua ambayo imekuwa na madhara makubwa kwa viumbe hai baharini.

Kwa upande wa Juliette Biao, mkurugenzi wa shirika la umoja wa mataifa kuhusu mazingira ukanda wa pwani, anasema mpango huu wa kulinda mazingira ya bahari, unafaa kuigwa na mataifa mengine ulimwenguni.

Hassan Shafi mmoja wa waliounda mashua hii, anasema kilichowavutia katika ubunifu huu ni takataka nyingi za plastiki ambazo zimekuwa zikipatikana katika mazingira ya bahari.

Mashua hiyo iliyoundwa na kikundi cha Plastic Revolution ilitengenezwa Kisiwani Lamu Kaskazini mwa pwani kwa kutumia plastiki na sasa iko safarini kuelekea visiwa vya pemba na Zanzibar nchini Tanzania.

Katika siku chahe zijazo boti hiyo itaanza safari kuelekea Pemba na Zanzibar na kurejea ilipotoka ambapo mafundi watajaribu kutafakari zaidi kuhusu namna bora ya matumizi ya boti hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.