Pata taarifa kuu
GABON-SIASA-AFYA

Rais wa Gabon Ali Bongo arejea nyumbani

Rais wa Gabon Ali Bongo yuko nyumbani nchini Gabon tangu jaan Jumatatu baada ya kuendeea kupewa matibabu kwa siku kadhaa nchini Morocco. Rais Ali Bongo anatarajia kuongoza leo Jumanne sherehe ya kuapishwa kwa serikali mpya, baada ya zaidi ya miezi miwili akiwa nje ya nchi.

Rais wa Gabon Ali Bongo Ondimba, Januari 29, 2018, à Addis Ababa, Ethiopia.
Rais wa Gabon Ali Bongo Ondimba, Januari 29, 2018, à Addis Ababa, Ethiopia. REUTERS/Tiksa Negeri
Matangazo ya kibiashara

Taarifa ya kurejea kwa rais ali Bongo nchini Gabon imethibitishwa na runinga ya taifa ya Gabon pamoja na familia yake.

"Madaktari wamebaini kwamba safari ya rais Ali Bongo kwenda Gabon si hatari kwa afya yake. familia yake imesema.

Bw Bongo amekuwa nje ya nchi hiyo kwa zaidi ya miezi miwili, akipokea matibabu nchini Morocco kutokana na maradhi ambayo hayajafichuliwa baada yake kuugua akiwa ziarani Saudi Arabia 24 Oktoba kuhudhuria mkutano mkubwa wa kiuchumi nchini humo.

Taarifa zinasema alikumbwa na kiharusi.

Familia ya Bongo imetawala taifa hilo kwa miaka 51 iliyopita, na imetuhumiwa kwa kujilimbikizia mali na utajiri mkubwa kutokana na rasilimali za taifa hilo.

Rais Ali Bongo alichukua madaraka ya kuiuongoza nchi hiyo kutoka kwa babab yake Omar Bongo mwaka 2009, ambaye aliiiongoza nchi hiyo ya Afrika Magharibi kwa zaidi ya miaka 40.

Rais Ali Bongo anarejea nchini diku chache baad aya utawala wake kuponea kuangushwa kufuatia jaribio la mapinduzi lilitibuliwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.