Pata taarifa kuu
DRC-AFYA-QUININE-HAKI

Maofisa wawili wakamatwa kwa kukutengeneza dawa bandia DRC

Maafisa wawili wa moja ya kampuni kubwa za dawa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wanazuiliwa baada ya kampuni yao kutengeneza dawa aina ya "Quinine bandia". Watu hawa wamekamatwa tangu siku ya Ijumaa wili iliyopita kwa ombi la mshauri maalum wa Rais wa DRC Joseph Kabila vyanzo rasmi vimebaini Jumatatu wiki hii.

Dawa aina ya Quinine ikitengenezwa Bukavu, mashariki mwa DRC, tarehe 5 Agosti 2002.
Dawa aina ya Quinine ikitengenezwa Bukavu, mashariki mwa DRC, tarehe 5 Agosti 2002. © AFP
Matangazo ya kibiashara

"Karkera Premanata, meneja mkuu wa kampuni Zenufa na Bw Tshikaya Kabengele Barthelemy, afisa anayehusika na kuuza dawa kwenye kampuni ya Zenufa, wanakabiliwa na mashitaka ya kuuza quinine bandia, kufoji vyeti," amesema katika barua iliyowasilishwa kwa mwendesha mashitaka mkuu wa Kinshasa

"Kutokana na kuepuka kutoroka, tumeamua kuendelea kuwashikilia, wawe mikononi mwa ofisi ya mashitaka ndani ya kipindi kinachoruhusiwa kisheria", mshauri maalum wa Rais Joseph Kabila amesema katika barua nyingine kwa mkaguzi wa mahakama.

Bw Luzolo Bambi amelithibitishia shirika la Habari la AFP uhalisia wa barua hizo.

Maafisa wawili wa Zenufa wanazuiliwa katika jengo la ofisi ya mashitaka ya Matete, kimebaini chanzo cha mahakama.

Zenufa SARL ni kampuni ya dawa kutoka India iliyoanzishwa nchini DRC tangu mwaka 1998. Quinine ni moja ya bidhaa kubwa za kampuni hii. Bidhaa hii inachukuliwa kuwa tiba bora zaidi ya malaria nchini DRC.

Malaria ni ugonjwa unaohatarisha maisha ya watu kutokana na vimelea vinavyoingizwa kwa binadamu kutokana na kuumwa kwa mbu ya kike, kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO).

Malaria inachukuwa mstari wa mbele kwa kusababisha vifo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kwa mujibu wa Mpango wa Kitaifa wa Udhibiti wa Malaria nchini DRC.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.