Pata taarifa kuu
CAMEROON-SIASA-USALAMA

Hatua ya Samuel Eto'o kumuunga mkono Paul Biya yazua sintofahamu Cameroon

Siku chache kabla ya uchaguzi wa urais nchini Cameroon, rais anayemaliza muda wake, Paul Biya, amepata uungwaji mkono kutoka kwa nyota wa soka wa Cameroon Samuel Eto'o.

Samuel Eto'o, hapa kwenye sherehe ya Ballon d'Or Januari 11, 2016, ametangaza kwamba anamuunga mkono Paul Biya kuwania katika uchaguzi wa urais, Cameroon.
Samuel Eto'o, hapa kwenye sherehe ya Ballon d'Or Januari 11, 2016, ametangaza kwamba anamuunga mkono Paul Biya kuwania katika uchaguzi wa urais, Cameroon. © FABRICE COFFRINI / AFP
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo rais Paul Biya pia amepata uungwaji mkono kutoka kwa nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya Cameoon, Rigobert Song.

Kwenye mitandao ya kijamii baadhi wamemtaja samuel Eto'o kama mtu asiefaa na muhaini, huku wengine wakitilia shaka uraia wake wakisema si raia wa Cameroon.

Samuel Etoo Fils amesema atampigia kura mgombea anaetetea Umoja na kuwatolea wito mashabiki wake kufanya kama yeye.

Hayo ni wakati mwanamuziki mashuhuri nchini humo Richard Bona ameukosoa utawala wa Paul Biya bila hata hivyo kutoa msimamo wake kuhusu mgombea ataempigia kura.

Rais wa sasa Paul Biya mwenye umri wa miaka 85 anatarajiwa kuchaguliwa tena kwa muhula wa sita katika uchaguzi uliopangwa kufanyika Octoba 7 mwaka huu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.