Pata taarifa kuu
DRC-UN-USALAMA-SIASA

Joseph Kabila aonya nchi za kigeni kungilia katika masuala ya DRC

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila Kabange ameonya nchi za kigeni kwa kile alichokitaja "kuingiliwa katika masuala ya nchi yake, na kuomba kwa mara nyingine Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini DRC (Monusco) kuondoka nchini humo.

Rais wa DRC Joseph Kabila kwenye jukwaa la Umoja wa Mataifa, Septemba 25, 2018.
Rais wa DRC Joseph Kabila kwenye jukwaa la Umoja wa Mataifa, Septemba 25, 2018. © REUTERS/Eduardo Munoz
Matangazo ya kibiashara

Kauli hiyo aliitoa katika mkutano Mkuu wa 73 wa Umoja w Mataifa huko New York nchini Marekani. Mkutano ambao ulianza tangu Jumanne wiki hii.

Joseph Kabila ameelezea ahadi yake kwa maadili yaliyotetewa na Umoja wa Mataifa, huku akishtumu baadhi ya nchi za kigeni kuingilia katika masuala ya ndani ya nchi yake.

Rais Kabila amesema DRc imekua sasa na amani na utulivu , huku akiomba akisisitiza Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini DRC (Monusco) kuanza kuondoa askari wake nchi humo.

Ni miaka ishirini baada ya kutumwa kwa vikosi vya Umoja wa Mataifa katika nchi yangu na kwa sababu ya matokeo yao ambayo si mazuri katika mpango wa operesheni za kijeshi, Serikali yangu inaomba ikisisitiza vikosi hivyo vya Umoja aw Kimataifa kuanza kuondoka.

Kauli hii inakuja wakati serikali ya DRC, hasa majeshi yake yameendelea kukosolewa kushindwa kudhibiti usalama katika maeneo mengi ya nchi, hasa katikamikoa ya Kivy Kaskazini, Kivu Kusini, na Tanganyika.

Baadhi ya askari wameshtumiwa kuhusika katika mauaji ya watu wasiokuwa na hatia katika maeneo mbalimbali, hasa katika mkoa wa Kasai na mji Kinshasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.