Pata taarifa kuu
CAMEROON-USALAMA

Askari wanne na polisi 1 wauawa Cameroon

Hali ya usalama inaendelea kudorora katika maeneo ya Wazungumza Kiingereza, Kaskazini Magharibi mwa Cameroon. Askari wanne na polisi mmoja, waliuawa Jumapili katika maeneo hayo, kwa mujibu wa shirika la habari la AFP likinukuu vyanzo vya usalama na mashahidi.

Askari wa KCameroon huko Buea, mji wa Cameroon wanakozungumza Kiingereza.
Askari wa KCameroon huko Buea, mji wa Cameroon wanakozungumza Kiingereza. ALEXIS HUGUET / AFP
Matangazo ya kibiashara

Katika Esu, kijiji cha kaskazini magharibi karibu na mji wa Wum, askari wanne waliuawa katika shambulio dhidi ya kambi jeshi, kulingana na chanzo kilio karibu na idara za usalama katika mkoa huo.

"Shambulio lilitokea asubuhi (Jumapili) na askari wapya walishutushwa na milio ya risasi zilizokua zikifyatuliwa na wanaharakati wanaotaka kujitengwa kwa maeneo yao, " chanzo hicho kimesema, na kuongeza kuwa watu kadhaa walijeuhiwa, lakini hakikutoa maelezo zaidi kuhusu idadi ya watu waliojeruhiwa.

Wakaazi wa Esu walitoroka makazi yao kutokana na mashambulio hilo, kwa mujibu wa mmoja wao. "Wengi wamekimbilia msituni kwa hofu ya kuuawa, wengine wanajaribu kwenda katika mji wa Bamenda", mji mkuu wa Jimbo la Kaskazini Magharibi, mkaazi huyo amesema.

Katika Mutengene, karibu na Buea, mji mkuu wa kusini-magharibi, polisi, Ekah Njume, aliuawa nyumbani kwake na watu wasiojulikana, kwa mujibu wa mashahidi. Taarifa hii imethibitishwa Jumatatu wiki hii na vyombo vya habari vya Cameroon.

Usalama katika mikoa miwili ya watu wanaozungumza Kiingereza umeendelea kudorora kwa kiasi kikubwa tangu mwishoni mwa mwaka 2017.

Polisi zaidi ya 80 wamepoteza maisha tangu kuzuka kwa mgogoro huo , ambao pia umesababisha takribani watu 195,000 kuyatoroka makaazi yao, ikiwa ni pamoja na 34,000 kukimbilia nchi jirani ya Nigeria.

Mapigano na mashambulizi ya makundi ya watu wenye silaha dhidi ya vikosi vya usalama yamekuwa yakishuhudiwa kila kukisha nchini Cameroon. Wanaharakati wanaotaka kujitenga kwa maeneo yao, wamegawanyika katika makundi mengi madogo madogo, na wanataka maeneo yao yawe taifa huru wanakozungumza Kiingereza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.