Pata taarifa kuu
NIGERIA-URUSI-USALAMA

Nigeria yataka kuwarejesha nyumbani raia wake waliokwama Urusi

Serikali ya Nigeria imetangaza kwamba inataka kuwarejesha nyumbani raia wake waliokwama nchini Urusi kwa kukosa pesa ya nauli baada ya kununua Fan ID, hati ambayo ilipelekea mashambiki kupata visa wakati wa Kombe la Dunia la soka nchini Urusi, kulingana na taarifa kutoka ofisi ya rais.

Mashabiki wa soka, raia waNigeria, wakiangalia mechi ya soka ya Kombe la Dunia kati ya Croatia na Nigeria mbele ya televisheni kubwa huko Lagos Juni 16, 2018.
Mashabiki wa soka, raia waNigeria, wakiangalia mechi ya soka ya Kombe la Dunia kati ya Croatia na Nigeria mbele ya televisheni kubwa huko Lagos Juni 16, 2018. © AFP
Matangazo ya kibiashara

"Rais Muhammadu Buhari ameamuru (...) kuanza mchakato wa kuwarejesha nchini Nigeria raia wa Nigeria ambao walikwenda Urusi kuhudhuria michuano ya Kombe la Dunia 2018 na walijikuta wamekwama baada ya michuano hiyo," alisema mmoja wa wasemaji wake. Garba Shehu.

Baadhi walikwama kwa siku kadhaa katika uwanja wa ndege wa Vnukovo mjini Moscow wakati wengine waliamua kupiga kambi mbele ya ubalozi wao katika mji mkuu wa Urusi.

Raia hawa wa Nigeria walinunulia hati hii (Fan ID) kwa Naira (fedha za Nigeria) 250,000 (sawa na euro 600) wakiwa na matumaini ya kuishi nchini Urusi na kufanya kazi huko, hata kujiunga na timu ya soka nchini humo. Lakini Fan ID hairuhusu mtu kuffanya kazi nchini Urusi, wala kuishi kwa muda mrefu nchini humo.

Wengine walisema kuwa walikuja tu nchini Urusi kuhudhuria michuano ya Kombe la Dunia, lakini mashirika bandia ya usafiri ambayo yaliwatapeli, yalifuta safari yao ya kurejea nyumbani na kuwaibia nauli yao.

Shirika llisilo la kiserikali Alternativa, ambalo linapambana dhidi ya biashara ya binadamu, linakadiria kwamba karibu watu 200 kutoka Nigeria walijikuta katika mkumbo huo mjini Moscow kwa sababu ya utapeli huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.