Pata taarifa kuu
ETHIOPIA-ERITREA-USHIRIKIANO

Eritrea na Ethiopia zatangaza kusitisha vita

Siku moja baada ya mkutano wa kihistoria wa viongozi wa nchi mbili jirani, Eritrea na Ethiopia, hatimaye viongozi hao wametia saini kwenye tamko la pamoja huko Asmara kuimarisha uhusiano wao na kusitisha miaka ishirini ya vita.

Rais wa Eritrea Issaias Afwerki na Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed huko Asmara, Eritrea, Julai 9, 2018.
Rais wa Eritrea Issaias Afwerki na Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed huko Asmara, Eritrea, Julai 9, 2018. Twitter/ Fitsum Arega
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Eritrea Issaias Afeworki na Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed wametia saini "tamko la pamoja la amani na urafiki" Jumatatu asubuhi katika mji mkuu wa Eritrea, Waziri wa Habari wa Eritrea, Yemane Gebremeskel, amesema.

Nakala hii inasema hasa kuwa "hali ya vita iliyo kuepo kati ya nchi hizo mbili imefikia mwisho, na wakati mpya wa amani na urafiki umewadia".

"Nchi zote mbili zitjikita katika kukuza ushirikiano wa karibu katika nyanja ya siasa, uchumi, kijamii, utamaduni na usalama," Waziri wa Habari wa Eritrea ameongeza.

Hati hiyo inathibitisha kuanzishwa upya kwa biashara, usafiri na mawasiliano ya simu, kufufuliwa kwa uhusiano wa kidiplomasia na utekelezaji wa mkataba wa kimataifa wa mwaka 2000 juu ya mpaka wa pamoja.

Picha za sherehe zinaonyesha rais Issaias na Waziri Mkuu Abiy wameketi kwenye dawati la mbao, na nyuma yao kukioneka bendera za nchi hizo mbili , wakitia saini tamko hilo la pampja. Muda mfupi baadaye, Bw Abiy aliondoka Eritrea kurudi Addis Ababa baada ya ziara ya siku mbili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.