Mvutano waendelea kujitokeza DRC kuelekea Uchaguzi mkuu
Wanaharakati wanaomuunga mkono rais Joseph Kabila nchini DRC wanaojiita FCC, wamezindua mkakati wa kisiasa kuelekea Uchaguzi Mkuu mwezi Desemba mwaka huu.
Imechapishwa:
Hata hivyo, hawajaeleza iwapo rais Kabila atawania muhula wa tatu kinyume cha Katubaya nchi hiyo, licha ya kuonekana kumtaka kufanya hivyo, baada ya kumtaja kuwa ndio kiongozi wao.
Wakati wa hotuba yake wakati wa kuadhimisha miaka 58 ya Uhuru mwishoni mwa juma lililopita, rais Joseph Kabila aliswahakikishia wananchi wa DRC kuwa Uchaguzi Mkuu wa mwezi Desemba utafanyika kama ilivyopangwa lakini, Maaskofu wa Kanisa Katoliki wanasema wana mashaka iwapo Uchaguzi huo utafanyika.
Uchaguzi nchini DRC umepangwa kufanyika mnamo mwezi Desemba, na mivutano ya kisiasa bado inaendelea kuhusu uchaguzi huo. Baadhi ya wanasiasa wa upinzani wanataka uchaguzi huo ufanyike bila Kabial kuepo. Na wengine wanataka rais Joseph Kabila ashiriki katika uchaguzi huo.