Pata taarifa kuu
DRC-CENI-UCHAGUZI-SIASA

CENI yaanzisha mchakato wa kuchapisha orodha ya wapiga kura DRC

Tume ya uchaguzi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo CENI kuanzia Jumatatu wiki hii itaanza kuweka wazi orodha ya majina ya wapiga kura katika uchaguzi uliopangwa kufanyika tarehe 23 mwezi Desemba.

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi DRC, Corneille Nangaa.
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi DRC, Corneille Nangaa. Ceni Kinshasa
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii inakuja siku mbili baada ya Jumuiya ya nchi zianazozungumza lugha ya Kifaransa “Francophonie” (OIF) kuitaka tume hiyo, CENI kuhakikisha inapitia upya orodha ya wapiga kura iliyokuwa na mamilioni ya majina yaliyojirudia ikiwemo watoto wadogo ambao hawastahili kushiriki kwenye uchaguzi.

Hayo yanajiri wakati ambapo hali ya mabishano na hasira imeendelea nchini DRC kufuatia mabango yenye picha ya rais Joseph Kabila, yakiwa na maandishi kuwa Kabila ni "mgombea" wa kiti cha urais katika uchaguzi wa Desemba 23.

Mabango hayo yaliyobuniwa na wafuasi wa chama tawala cha PPRD yameonekana katika maeneo ya umma, kama vile Soko la Lalu, katika wilaya ya Binza Delvaux, magharibi mwa jiji kuu Kinshasa.

Wadadisi wa mambo wanaona kuwa mpango huo ulioanzishwa na chama hicho ni “mkakati hatari" kwa mchakato wa uchaguzi nchini humo.

Hivi karibuni vyama vya upinzani na mashirika ya kiraia walipinga orodha ya vyama 599 na miungano 77 ya vyama vya kisiasa vilivyoruhusiwa kufanya shughuli zao nchini DRC, na ambavyo vitaweza kushiriki katika uchaguzi wa mwezi Desemba 2018, baada ya kuchapishwa kwenye Jarida la serikali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.