Pata taarifa kuu
NIGER-USALAMA

Afisa wa shirika la kihisani atekwa nyara Niger

Afisa wa shirika la kutoa misaada kutoka Ujerumani anaendelea kushikiliwa na kundi la watu wenye silaha ambao hawajulikani walipo, baada ya kukimbilia nchini Mali.

Afisa wa shirika la kutoa misaada kwa wakimbizi wa Mali alitekwa nyara nchini Niger na kupelekwa kwenye mpaka wa Mali.
Afisa wa shirika la kutoa misaada kwa wakimbizi wa Mali alitekwa nyara nchini Niger na kupelekwa kwenye mpaka wa Mali. Google map
Matangazo ya kibiashara

Afisaa huyo alitekwa nyara siku ya Jumatano, Aprili 11, kaskazini mwa mji mkuu wa Niger, Niamey, katika jimbo la Ayorou. Alikua akifanya kazi kwa shirika lisilo la kiserikali la Help, linalohudumia wakimbizi kutoka Mali.

Afisa huyo alikuwa akitembea kwenye mtaa wa 18, katika eneo hatari, bila kusindikizwa na askari, wakati alitekwa.

Kundi la watu wenye silaha ambao walikua kwenye pikipiki ndio waliomteka nyara, baada ya kuzingira gari lake kilomita 25 kusini mwa mji wa Inatès, karibu na mpaka wa Mali.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka eneo hilo, mfanyakazi huyo wa shirika la Help, ambaye alikua pamoja na raia wanne kutoka Niger, hakutoa upinzani wowote alipotekwa nyara.

Kabla ya kukimbilia kuelekea mpaka wa Mali, watekaji nyara hao walichoma moto gari la shirika hilo lisilo la kiserikali, na kuwashikilia kwa muda wa masaa kadhaa raia wanne wa Niger ikiwa ni pamoja na mwanamke, kabla ya kuwaachilia karibu na gari hilo lililokuwa likiteketea kwa moto.

Sio mara ya kwanza afisa huyu ambaye husaidia wakimbizi wa Mali kutembelea

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.