Pata taarifa kuu
ZIMBABWE-MUGABE-SIASA

Mugabe: Waliniondoa madarakani kijeshi

Rais wa zamani wa Zimbabwe Robert Gabriel Mugabe amesema kuondoka kwake ofisini mwezi Novemba mwaka jana kulikuwa ni mapinduzi ya kijeshi na kutoa wito wa hali hiyo kubadilishwa.

Rais wa zamani wa Zimbabwe  Robert Mugabe
Rais wa zamani wa Zimbabwe Robert Mugabe REUTERS/Mike Hutchings/File Photo
Matangazo ya kibiashara

Mugabe ametoa kauli hii kwenye mahojiano yake ya kwanza ya televisheni tangu ang’olewe madarakani na nafasi yake kuchukuliwa na rais wa sasa Emmerson Mnangagwa.

Aidha, Mugabe amesisitiza kuwa kilichofanyika ni mapinduzi ya kijeshi na kudai kuwa mrithi wake rais Mnangagwa asingeweza kuwa rais wa taifa hilo kama asingepata msaada wa jeshi.

Kauli ya Mugabe imekuja wakati huu wanaharakati kadhaa wakienda Mahakama ya Katiba kutaka kubatilishwa kwa namna rais Mnangagwa alivyoingia madarakani wakisema alitumia jeshi kupindua Serikali halali.

Hata hivyo, Mugabe amesema hataki tena kuwa rais wa nchi hiyo licha ya kutoa malalamishi haya.

“Sitaki tena kuwa rais, sasa hivi nina miaka 94,” alisema rais Mugabe.

“Watu wanastahili kuchaguliwa serikalini kwa njia mwafaka. Niko tayari kwa majadiliano.Nitasaidia katika hilo lakini lazima nialikwe,”aliongeza Mugabe.

Uchaguzi Mkuu unatarajiwa kufanyika mwezi Agosti mwaka huu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.