Pata taarifa kuu
NIGERIA-WHO-LASSA

Watu 110 wapoteza maisha nchini Nigeria baada ya kuambukizwa homa ya Lassa

Homa iliyopewa jina la Lassa imesababisha vifo vya watu 110 nchini Nigeria kuanzia mwaka huu.

Virusi vya Lassa vikionekana kwa karibu
Virusi vya Lassa vikionekana kwa karibu CDC's Public Health Image Library
Matangazo ya kibiashara

Takwimu hizi zimetolewa na kituo cha kudhibiti magonjwa nchini humo.

Maambukizi haya yaliripotiwa mara ya kwanza nchini humo mwaka 2016.

Tangazo hili limekuja baada ya wiki iliyopita, Shirika la afya duniani WHO kusema kuwa watu 317 walikuwa wameambukizwa homa hii.

Kati ya watu 1,121 waliokwenda kupima hivi karibuni, zaidi ya 300 wameambukizwa huku wengne 700 wakipatikana bila maambukizi hayo.

Serikali ya Nigeria inasema homa hiyo imeathiri majimbo 18 kati ya 36 na huku maafisa wa afya 16 wakiambukizwa.

Dalili za homa hiyo ni pamoja na kutapika, kutokwa damu katika maeneo yaliyo wazi ya mwili na kupata joto kupita kiasi.

Homa hiyo ambayo iliripotiwa mara ya kwanza nchini humo katika mji wa Lassa mwaka 1969, umewekwa pamoja na magonjwa ya Marburg na Ebola, ambayo hayana dawa.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.