Pata taarifa kuu
BURKINA FASO-UGAIDI-UFARANSA

Hali ya kawaida yarejea katika Ubalozi wa Ufaransa jijini Ouagadougou

Hali imerejea kama kawaida katika Ubalozi wa Ufaransa jijini Ouagadougou nchini Burkina Faso baada ya wavamizi wanne waliokuwa wamekwenda kuvamia Ubalozi huo wa nchi hiyo, kituo cha utamaduni na makao makuu ya jeshi nchini humo.

Uvamizi katika Ubalozi wa Ufaransa jijini Ouagadougou
Uvamizi katika Ubalozi wa Ufaransa jijini Ouagadougou Ahmed OUOBA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Serikali ya Burkina Faso imethibitisha kuuawa kwa wavamizi hao ambao kwa mujibu wa watu walioshuhudia, watu watano waliokuwa wamejihami kwa silaha walishuka ndani ya gari na kujaribu kushambulia Ubalozi huo.

Waziri wa Mambo ya nje wa Ufaransa Jean-Yves Le Drian amesema hakuna raia yeyote wa Ufaransa aliyejeruhiwa katika tukio hilo na taasisi zote za serikali ya Ufaransa zipo salama.

Baada ya shambulizi hili, Ubalozi wa Ufaransa nchini humo umewaambia raia wake kusalia nyumbani huku rais Emmanuel Macron akisema amekuwa akifahamishwa yale yote yaliyokuwa yanafanyika.

Shambulizi hili limekuja wakati huu Ufaransa ikiwa katika mstari wa mbele kuyasaidia mataifa katika ukanda wa Sahel ikiwemo Burkina Faso kupambana na makundi ya kjihadi.

Ufarans imetuma wanajeshi wake 4,000 katika mataifa hayo ambayo pia yanaundwa na Chad, Mali, Mauritania na Niger.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.