Pata taarifa kuu
ZIMBABWE-SIASA-USALAMA

Robert Mugabe aonekana hadharani Harare

Rais Robert Mugabe alionekana hadharani kwa mara ya kwanza leo Ijumaa asubuhi, siku mbili baada ya jeshi kuchukua udhibiti wa nchi hiyo. Shirika la habari la Reuters limearifu kuwa Mugabe alishangiliwa wakati wa sherehe baada ya kuzungumza.

Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe, Februari 15, 2017, Harare.
Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe, Februari 15, 2017, Harare. REUTERS/Philimon Bulawayo
Matangazo ya kibiashara

Mugabe ambaye alikua chini ya kizuizi cha nyumbani alionekana akihudhuria ya kuhitimu kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu mjini Harare. Alionekana akiwa huru wakati ambapo wengi walidhani kuwa bado yuko chini ya kifungo cha nyumbani.

Bw. Mugabe alihudhuria sherehe iliyoandaliwa na Chuo Kikuu cha Zimbabwe Open mjini Harare. Alivaa mavazi ya chuo kikuu ya manjano, toga ya bluu na kichwa kinachofanana. Inaonekana kama risasi halisi ya risasi.

Kwa hali hiyo Robert Mugabe alionyesha kuwa yuko huru na bado ni rais wa Zimbabwe na haja achia ngazi. Upande wa jeshi ambao walisema tangu awali kwamba haya si mapinduzi, ujumbe wao uko wazi. "Mnamuona rais yuko huru, hatukufuta Katiba. Tuko katika kwenye meza ya mazungumzo, ufumbuzi utapatikana".

Siku ya Alhamisi Mugabe alikutana na ujumbe kutoka Afrika Kusini uliotumwa na rais Jacob Zuma, mwenyekiti wa sasa wa Jumuiya ya nchi za kanda ya kusini mwa Afrika (SADC) pamoja na viongozi wa kijeshi, lakini hakuna taarifa rasmi iliyotolewa kuhusu mazungumzo hayo.

Hata hivyo Rais Mugabe anaripotiwa kukataa kuachia ngazi licha ya kuongezeka wito wa kumtaka ajiuzulu.

Vyanzo vya kuaminika vinasema kumekuepo na makubaliano, lakini huenda wameshindwa kuafikiana kuhusu tarehe ya Rais Mugabe kuachia ngazi.

Inaonekana kuwa itakua vigumu kukubaliana kuhusu tarehe ya kuondoka kwa Robert Mugabe mara baada ya mkutano wa chama cha tawala cha Zanu-PF mwezi ujao, au baada ya uchaguzi wa urais uliopangwa kufanyika mwaka ujao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.