Pata taarifa kuu
DRC-USALAMA

Hali ya utulivu yarejea, watu waendelea kuwa na hofu mjini Goma

Hali ya utulivu imeanza kurejea mjini Goma Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo baada ya watu wanne akiwemo afisa mmoja wa polisi kupoteza maisha siku ya Jumatatu.

Wakazi wa Goma wanasema wana hofu ya usalama wao kufuatia mgogoro wa kisiasa unaoendelea nchini DRC.
Wakazi wa Goma wanasema wana hofu ya usalama wao kufuatia mgogoro wa kisiasa unaoendelea nchini DRC. RFI/Leonora Baumann
Matangazo ya kibiashara

Watu hao walipoteza maisha katika maandamano na majibizano ya kumtaka rais Joseph Kabila kuondoka madarakani kufikia mwisho wa mwaka huu.

DRC imeendelea kuwa katika sintofahamu ya kisiasa, baada ya Tume ya Uchaguzi kusema kuwa haiwezi kuandaa uchaguzi mwaka huu kwa mujibu wa mkataba wa kisiasa uliofikiwa mwaka uliopita.

Akiwa ziarani nchini DRC wiki iliyopita, balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa, Nikki Haley, alisema kuna haja kwamba uchaguzi ufanyike mwaka ujao kinyume na ambavyo Tume ya uchaguzi CENI ilivyotangaza, kauli ambayo aliitoa punde baada ya kukutana na Mwenyekiti wa tume hiyo Corneille Nangaa mjini Kinshasa siku ya Ijumaa ya oktoba27.

Mgogoro wa kisiaa nchini DRC umesababisha vifo vya watu wengi na wengine kukamatwa. Baadhi ya watu wanaozuliwa jela kufuatia kuzuka kwa mgogoro huo mpaka sasa hawajafikishwa mbele ya vyombo vya sheria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.