Pata taarifa kuu
CONGO BRAZZAVILLE-UN

UN kuwarudisha nyumbani askari 600 wa Congo-Brazzaville

Hatimaye Umoja wa Mataifa umefikia maamuzi ya kuwarudisha nyumbani wanajeshi 600 wa Congo Brazzaville wanaohudumu katika kikosi cha kulinda amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Askari wa Umoja wa mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati (Minusca) wakipiga doria katika mitaa ya mji wa  Bangui Desemba 10, 2015.
Askari wa Umoja wa mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati (Minusca) wakipiga doria katika mitaa ya mji wa Bangui Desemba 10, 2015. MARCO LONGARI / AFP
Matangazo ya kibiashara

Umoja wa Mataifa unasema baada ya wanajeshi hao kubainika kuwa walihusika katika visa vya unyanyasaji wa kingono, ufisadi na utovu wa nidhamu, rais wa Congo Brazzaville Denis Sassou Nguesso amekubali ombi la umoja huo kuwarudisha nyumbani wanajeshi hao.

Jeshi hilo la kulinda amani la MINUSCA lenye wanajeshi 12, 000 limekuwa likikumbwa na visa vya utovu wa nidhamu tangu kwenda katika nchi hiyo mwaka 2014.

Wanajeshi hao wanahusishwa visa hivyo wanajiandaa kurudishwa nyumbani, lakini haijafahamika kwamba mahakama ya kijeshi ya Congo Brazzaville itashughulikia kesi hiyo, askari hao watakaposili nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.