Pata taarifa kuu
CHAD-SENEGAL-HABRE-HAKI

Uamuzi kuhusu kesi ya Hissene Habre kutolewa Alhamisi

Nchini Senegal, Mahakama inatazamiwa kutoa uamuzi wake Alhamisi hii Aprili 27, 2017 kuhusu kesi ya rais wa zamani wa Chad Hissene Habre. Baada ya miaka 20  akishikiliwa, uamuzi kuhusu rufaa aliyokataa utatolewa na mahakama ya rufaa, nchini Senegal.

Hissene Habre akizungukwa na wanajeshi baada ya kusikilizwa, Julai 2, 2013, Dakar.
Hissene Habre akizungukwa na wanajeshi baada ya kusikilizwa, Julai 2, 2013, Dakar. © .AFP/Stringer
Matangazo ya kibiashara

Mahakama ya mwanzo ilimuhukumu kiongozi huyo kifungo cha maisha jela kwa uhalifu wa kivita, uhalifu dhidi ya ubonadamu, mateso na ubakaji. Huenda mahakama ikathibitisha kifungo cha maisha jela, au kumpunguzia kifungo hicho au pia kumfutia mashitaka dhidi yake na kumuachia huru, kama walivyoomba wanasheria wake. Hakuna rufaa iitakayowezekana tena.

"Huu ni mwisho sasa wa mchakato mrefu wa kesi hiyo, amesema Marcel Mendy, msemaji kitengo cha mahakama ya Afrika nchini Senegal, hakuna rufaa yoyote ambayo itawezekana tena. Huu ni mwisho wa kesi hiyo, " ameongeza Bw Mendy.

Kesi ya Hissene Habre,imechukua muda wa miaka 20 ikisikilizwa.

Wanasheria wa Hissene Habre wanasubiri uamuzi wa mahakama. "Bado tuna shaka, najua kwamba majaji watathibitisha kifungo cha maisha jela kwa Hissene Habre", amesema Jacqueline Moudeina, mmoja wa wanasheria wake

Hissene Habre hajawahi kuimtambua mahakama hii maalumu iliyowekwa nchini Senegal na Mahakama ya Kimataifa mwaka 2012. Wanasheria wake walilalamika mara kadahaa wakisem akuwa kesi hiyo iligubikwa na makosa mengi na waliomba mteja wao aachiliwe huru. haijafahamika iwapo Hissene Habre atafika mahakamni kusikiliza uamuzi wa mahakama. Itafahamika kwamba Hissene Habre alisalia kimya mara mbili wakati kesi yake ilipokua ikisikilizwa na kukataa kuripoti mahakamani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.