Pata taarifa kuu
DRC

OCHA yasema hali ya kibinadamu ni mbaya jimboni Kasai nchini DRC

Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayotoa misaada ya kibinadamu (OCHA), inasema hali ya kibinadamu ni mbaya katika jimbo la Kasai nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Nembo ya jimbo la DRC ikionesha sehemu ya Kasai
Nembo ya jimbo la DRC ikionesha sehemu ya Kasai Wikipedia
Matangazo ya kibiashara

Hali hii imeendelea kushuhudiwa kwa sababu ya mauaji ya zaidi ya watu 400 ambayo yamekuwa yakishuhudiwa katika eneo la Kati ya nchi hiyo tangu mwezi Agosti mwaka uliopita.

OCHA inasema watu wengine 600,000 wameyakimbia makwao kwa sababu ya hali hii na wanahitaji msaada wa haraka.

Mbali na wakimbizi hao wa ndani kwa ndani, inaelezwa kuwa watu wengine Milioni 1.7 katika mikoa mingine kama Kasai-Oriental, Kasai, Lomami na Sankuru, pia wanahitaji misaada hiyo.

Mapigano makali kati ya waasi wa Kamuina Nsapu na wanajeshi wa serikali wamekuwa wakikabiliana tangu kuuawa kwa kiongozi wa waasi hao mwaka uliopita na huzua hali ya wasiwasi.

Mwezi Machi, polisi 39 waliuawa baada kushambuliwa na waasi wa Kamuina Nsapu.

Mbali na maafisa wa polisi, wafanyikazi wawili Umoja wa Mataifa kutoka Marekani na Sweden walitekwa na kuuawa katika eneo la Kasai.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.