Pata taarifa kuu
ZIMBABWE-MUGABE-SIASA

Mugabe: Grace Mugabe ana ushawishi mkubwa kisiasa

Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe, ambaye aliyesheherekea Jumanne wiki hii miaka 93 ya kuzaliwa kwake, bado anakabiliwa na mvutano ndani ya chama chake cha Zanu PF. Vita vya kuchukua nafasi yake vimeendelea kushuhudiwa, huku kukiwa na mvutano kuhusu umri wake mkubwa ukiendelea kukigawanya chama hicho.

Robert Mugabe Februari 21, 2015, akisherehekea miaka 91 ya kuzaiwa.
Robert Mugabe Februari 21, 2015, akisherehekea miaka 91 ya kuzaiwa. Philimon Bulawayo/Reuters
Matangazo ya kibiashara

Jumatano hii, Februari 22, katika mitaa ya Bulawayo, mji wa pili kwa ukubwa nchini Zimbabwe, vichwa vingi vya habari vinaonyesha hali ya sintofahamu katika chama tawala cha Zanu PF kutokana na mtu ambaye anaweza kumrithi Rais Robert Mugabe. Magazeti yanaelezea hasa kauli ya mwisho ya Rais Mugabe akimsifu mkeweGrace Mugabe, mwenye umri wa miaka hamsini na moja.

Kauli hiyo imewashangaza wengi nchini Zimabwe.

Katika mahojiano kwenye televisheni ya taifa katika siku yake ya kuzaliwa, Rais Mugabe alimsifu mkewe kuwa ni "moto wa kuotea mbali kisiasa na sasa ana uwezo wa kukabiliana na mvutano wa kisiasa ndani ya chama."

Rais Robert Mugabe, mwenye umri wa miaka 93, anakabiliwa na upinzani mkali ndani ya chama chake, kufuatia umri wake.

Wakati ambapo amekua akidai mara kwa mara kwamba haoni mtu hata mmoja miongoni mwa mawaziri wake na washirika wake wa karibu, ambaye anaweza kumrithi, Rais Robert Mugabe anaonekana kubadilisha mfumo na na kusem akwa upole kwamba kuna uwezekano wa kukabidhiana madaraka. Mugabe ambaye anatawala sasa kwa miaka 37amemtaja mkewe kwamba "ana ushawishi mkubwa kisiasa" na amemwita "Daktari Amai," ikimaanisha mama katika lugha ya Shona.

Grace Mugabe kwa sasa anaongoza kundi la wanawake wa chama tawala cha Zanu PF.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.