Pata taarifa kuu
SOMALIA-UCHAGUZI

Wabunge nchini Somalia kumchagua rais siku ya Jumatano

Wabunge nchini Somalia watapiga kura kumchagua rais siku ya Jumatano mjini Modagishu.

Mzee wa Kisomalia akisaidiwa kupiga kura katika siku zilizopita
Mzee wa Kisomalia akisaidiwa kupiga kura katika siku zilizopita Simon Maina/AFP
Matangazo ya kibiashara

Wagombea 23 wanawania wadhifa huo akiwemo rais wa sasa Hassan Sheikh Mohamoud.

Uchaguzi huu umekuwa ukiahiarishwa mara kwa mara tangu mwezi Agosti mwaka uliopita, hasa kwa sababu za kiusalama lakini pia baada ya kucheleweshwa pia kwa uchaguzi wa wabunge.

Wagombea wengine ni pamoja na Waziri Mkuu Omar Abdirashid Sharmarke, rais wa zamani wa serikali ya mpito Sheikh Sharif Ahmed na aliyekuwa Waziri Mkuu wake Mohamed Abdullahi Farmaajo.

Wabunge 275 ndio watakaopiga kura wakishirikiana na Maseneta 54 katika eneo maalum katika uwanja wa ndege mjini Mogadishu.

Siku ya Jumatano, safari za ndege zitasitishwa kuingia na kutoka mjini Mogadishu kutokana kwa sababu za kiusalama wakati wa zoezi hilo.

Wagombea wote 23 ni wanaume baada ya mgombea pekee wa kike kujiondoa mwaka uliopita.

Kila mgombea amelipa Dola za Marekani 30,000 kama ada ya kushiriki katika uchaguzi huu muhimu.

Atakayechaguliwa atakuwa na kazi kubwa ya kuhakikisha kuwa usalama unarejea nchini humo kutokana na tishio la Al Shabab, lakini pia kukabiliana na baa la njaa.

Suala la ufisadi pia limeendelea kuwa sugu nchini humo.

Kutokana na hali mbaya ya usalama, raia wa Somalia bado hawajapa fursa ya kumchagua kiongozi wao kwa kupiga kura kama ilivyo katika mataifa mengine.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.