Pata taarifa kuu
SOMALIA-KENYA-UN-HAKI

Mahakama ya ICJ kusikiliza kesi kati ya Somalia na Kenya kuhusu eneo la bahari

Mahakama ya juu kabisa ya umoja wa Mataifa, imekubali kusikiliza kesi iliyofungulia na nchi ya Somalia dhidi ya majirani zake nchi ya Kenya, kuhusu eneo la bahari ambalo linagombewa na nchi hizo mbili na linaelezwa kuwa na hifadhi kubwa ya mafuta na gesi.

Rais wa Somalia Hassan Cheikh Mohamoud, hapa ili kua Februari 14, 2016  nchini.
Rais wa Somalia Hassan Cheikh Mohamoud, hapa ili kua Februari 14, 2016 nchini. THOMAS KIENZLE / AFP
Matangazo ya kibiashara

Utawala wa Nairobi umeiambia mahakama ya kimataifa ya usuluhishi wa mipaka kuwa, haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo iliyofunguliwa na Serikali ya Somalia mwaka 2014.

Hata hivyo rais wa mahakama hiyo ya ICJ, Ronny Abraham, amesema kuwa hoja ya nchi ya Kenya kuhusu mipaka ya mahakama hiyo haina msingi na inapaswa kutupiliwa mbali.

Serikali ya Mogadishu ilifungua kesi hiyo, ikitaka mahakama hiyo iteo uamuzi wa kurudiwa kuchorwa kwa mpaka wa eneo la bahari wanalogombea, hatua ambayo ikiwa itafanyika huenda ukachukua sehemu kubwa ya eneo la Pwani ya Kenya ambalo lina hifadhi ya mafuta na gesi.

Somalia inasema imeamua kwenda kwenye mahakama hiyo baada ya mazungumzo kati yake na Kenya kushindikana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.