Pata taarifa kuu
MISRI-VYOMBO VYA HABARI-QATAR

Mwandishi wa habari wa Al-Jazeera akamatwa nchini Misri

Kituo cha habari cha Qatar cha Al-Jazeera kimetangaza kukamatwa kwa mwanahabari wake Mahmoud Hussein nchini Misri na kuwekwa rumande kwa siku 15. Uhusiano kati ya Misri na Qatar ulidorora baada ya jeshi la Misri kumng'atua madarakani rais Mohamad Morsi mwezi Julai 2013.

Matangazo ya runinga ya Al-Jazeera.
Matangazo ya runinga ya Al-Jazeera. livestation.com/en/aljazeera-mubasher-misr
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa Ofisi ya mashitaka ya Misri, Mahmoud Hussein anatuhumiwa kutaka "kuipindua serikali kwa njia ya filamu za uzushi kuhusu hali ya kijamii na kiuchumi nchini Misri."

Chanzo kilio karibu na uchunguzi kinabaini kwamba, wanataka kujua sababu za kuandaa au kutengeneza filamu hiyo ijulikanayo kwa jina la "al' asaker", "askari", iliyorushwa hewani kwenye runinga ya Al-Jazeera mwezi Novemba 2016. Filamu hiyo, inayodaiwa kwamba ilitengenezwa vibaya, iliibua hasira kali kwa serikali ya Misri lakini pia hasiri kwa baadhi ya raia wa nchi hiyo.

Raia wengi wa Misri walipewa mafunzo ya kijeshi. Serikali ya Misri inaona kwamba filamu hii ilitengezwa kwa minajili ya kuhamasisha raia wa Misri kuchukua silaha na kupambana dhidi ya utawala uliopo madarakani.

Si mara ya kwanza Misri kuwaweka mbaroni waandishi wa habari wa kituo cha habari cha Al-Jazeera. Misri iliwahi kuwakamata na kuwazuia jela waandishi wa habari wa kituo hiki, hali iliyopelekea Misri kukosolewa kimataifa kwa kuminya uhuru wa vyombo vya habari.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.