Pata taarifa kuu
GAMBIA-UFARANSA

Ufaransa yamtaka rais Jammeh kuondoka madarakani haraka

Rais wa Ufaransa Francois Hollande amemtaka rais wa Gambia Yahya Jammeh kukubali kuwa alishindwa kwenye Uchaguzi wa urais uliofanyika mapema mwezi huu.

Rais wa Ufaransa François Hollande
Rais wa Ufaransa François Hollande REUTERS/Eric Vidal
Matangazo ya kibiashara

Aidha, Hollande amemtaka Jammeh ambaye ameongoza nchi yake kwa miaka 22, kuondoka madarakani na kumwachia madaraka rais mteule Adama Barrow.

Kiongozi huyo wa Ufaransa ambaye ametangaza kutowania muhula wa pili wakati wa Uchaguzi wa urais nchini mwake mwaka 2017, amesisitiza kuwa matokeo ya Uchaguzi wa Gambia yalikuwa huru, wazi na haki.

“Matokeo ya Desemba tarehe 1 yalikuwa ya haki na ni lazima Adama Barrow aapishwe haraka iwezekanavyo,” amesema Hollande.

Wito kama huo pia umetolewa na Mabalozi 11 wa Gambia wanaowakilisha nchi zao katika nchi mbalimbali duniani.

Mabalozi hao wa Gambia nchini Marekani, China, Uingereza, Urusi,Ubelgiji na mataifa mengine, wamemwadikia barua Jammeh kumwomba kumwachia madaraka mpinzani wake na kumpongeza kwa ushindi.

Juhudi za viongozi wa nchi za Afrika Magharibi ECOWAS kumshawishi Jammeh kuondoka madarakani hazijazaa matunda.

Rais Jammeh alikuwa amekubali kushindwa lakini akabadilisha mawazo baada ya wiki moja.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.