Pata taarifa kuu
GAMBIA-ECOWAS

Ujumbe wa ECOWAS ziarani Banjul

Jumuiya ya Kiuchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi (ECOWAS) itatuma, Jumanne Desemba 13, ujumbe mjini Banjul, mji mkuu wa gambia kumshawishi Yahya Jammeh kuachia madaraka.

Rais anayemaliza muda wake nchini Gambia Yahya Jammeh aendelea kukataa matokeo ya uchaguzi yaliyotangazwa na Tume ya Uchaguzi nchini Gambia..
Rais anayemaliza muda wake nchini Gambia Yahya Jammeh aendelea kukataa matokeo ya uchaguzi yaliyotangazwa na Tume ya Uchaguzi nchini Gambia.. REUTERS/Carlos Garcia Rawlins/Files
Matangazo ya kibiashara

Baada ya kushindwa katika uchaguzi wa Urais wa Desemba 1, na kumpongeza mshindani wake Adama Barrow aliyeibuka msindi, rais Yahya Jammeh alirejelea kauli yake siku mbili zilizopita na kutangaza kwamba hakubali matokeo ya uchaguzi.

Ujumbe wa ECOWAS utaongozwa na rais wa Liberia, Ellen Johnson Sirleaf, na atakua pamoja na wenzake wa Nigeria, Muhammadu Buhari, Sierra Leone, Ernest Bai Koroma, na Ghana, John Dramani Mahama, chanzo cha kidiplomasia kutoka Senegal kimebaini. Ujumbe huo una matumaini ya kumshawishi Yahya Jammeh kuachia madaraka, chanzo hicho kimeongeza.

Licha ya shinikizo kubwa ya kimataifa, Yahya Jammeh amewashangaza wengi baada ya kutangaza kwamba atapinga matokeo ya uchaguzi urais mbele ya Mahakama Kuu.
Itafahamika kwamba Desemba 2 rais Yahya Jammeh alikubali kuwa alishindwa katika uchaguzi huo na kumpongeza mshindani wake Adama barrow kwa kuibuka mshindi.

Hata hivyo Mwenyekiti wa Tume ya ECOWAS ameiambia RFI kwamba watajaribu kumshinikiza rais Yahya Jammeh na kama ataendelea kupinga kuna uwezekano wa kuingilia kijeshi nchini Gambia.

"Diplomasia inapewa kipaumbele" ili rais wa Gambia Yahya Jammeh "akubali matokeo ya uchaguzi," lakini kuingilia kijeshi "inawezekana katika hatua ya mwisho," Mwenyekiti wa Tume ya ECOWAS amesema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.