Pata taarifa kuu
ALGERIA-WAHAMIAJI

Wahamiaji wafukuzwa nchini Algeria

Kwa ujumla, wahamiaji 1400 wanaochukuliwa kama wahamiaji haramu watafukuzwa nchini Algeria, uamuzi huo umechukuliwa na serikali ya nchi hiyo.

Wahamiaji kutoka Niger, wachukuliwa kama wahamiaji haramu nchini Algeria, katika mji wa Boufarik, mwaka 2014.
Wahamiaji kutoka Niger, wachukuliwa kama wahamiaji haramu nchini Algeria, katika mji wa Boufarik, mwaka 2014. AFP PHOTO/FAROUK BATICHE
Matangazo ya kibiashara

Shirika hilo limesema kuwa wahamiaji ambao wengi wao ni kutoka Afrika Magharibi, walikamatwa katika nyumba zao na polisi Alhamisi wiki iliyopita mjini Algiers.

Shirika hilo linalotetea haki za binadamu limesikishwa kuwaona wanawake wajawazito na watoto miongoni mwa wahamiaji ambao watafukuzwa nchini Algeria.

Kulikuwa na watu waliojeruhiwa miongoni mwa wahamiaji, kwa mujibu wa shirika hilo la haki za binadamu, taarifa ambayo haijathibitishwa na serikali.

Serikali ya Algeria ilitangaza operesheni hiyo tangu mwezi Septemba.

Hivi karibuni, mapigano kati ya wahamiaji na raia wa Algeria yalitokea kusini mwa nchi hiyo kwa sababu ya viwango vya ukosefu wa ajira kuwa juu zaidi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.