Pata taarifa kuu
DRC-USALAMA

DRC: watu wasiopungua 13 wauawa katika ghasia za kikabila

Kwa uchache watu 13 wameuawa katika ghasia zilizotokea katika baadhi ya vijiji wilayani Kabalo mkoani Tanganyika tangu Jumapili Oktoba16. Ghasia hizo ni kati ya makabila mawili ya Wabantu na Mbilikimo.

Watu walioyahama makazi yao kutokana na vurugu katika mji wa Katanga, DRC.
Watu walioyahama makazi yao kutokana na vurugu katika mji wa Katanga, DRC. DR / Refugees International
Matangazo ya kibiashara

Tangu mwaka 2013, vurugu kati ya makabila ya Mbilikimo na Waluba zimekua zikitokea mara kwa mara kaskazini mwa mkoa wa zamani wa Katanga. Mapigano yaliyoikumba tangu mwezi Agosti mwaka jana wilaya jirani ya Nyunzu na kusababisha maelfu ya watu kuyahama makazi yao, bado zimo vichwani mwa watu.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, watu kutoka jami za Mbilikimo na Waluba walikabiliana kwa kutumia mishale na fimbo katika wilaya ya Kabalo. Hali hiyo ilizuka baada ya watu kutoka jamii ya Mbilikimo kutozwa kodi kwa Viwavi ambao wanawatumia kama chakula.

Viwavi huwa ni chakula cha raia wengi wa wanaoishi magharibi mwa Jmhuri ya Kidemokrasia ya Congo karibu na eneo lililo karibu na mji mkuu Kinshasa, ambapo ni karibu na mji wa Katanga.

Wadudu hao huchukuliwa kutoka kwa miti, huchomwa na kuliwa na mchuzi.Viwavi hawawezi kusababisha vita vya mara kwa mara katika taifa hilo hususan eneo la Katanga.

Mbilikimo ndio wanaotoka wanahisi wamebaguliwa kwa kukosa mali asili na elimu.

Kwa hivyo walipohisi kwamba chanzo kimoja cha mapato yao kinawekewa kodi,matokeo yakawa vita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.