Pata taarifa kuu
CONGO-MVUTANO

Mvutano waongezeka katika mkoa wa Pool

Upinzani umebaini kupelekwa kwa vikosi vya usalama katika mkoa wa Pool nchini Congo-Brazzaville tangu mwishoni mwa wiki iliyopita. Uwepo wa wanajeshi na askari polisi pembezoni na eneo la Mayama, makao makuu ya Mchungaji Frédéric Bintsamou, mmoja wa viongozi wa upinzani umesababisha raia kukimbiliaa msituni.

LMchungaji Frédéric Bintsamou almaarufu "Ntumi" Juni 20, 2007 katika mji wa Kinkala kusini mwa Congo.
LMchungaji Frédéric Bintsamou almaarufu "Ntumi" Juni 20, 2007 katika mji wa Kinkala kusini mwa Congo. AFP
Matangazo ya kibiashara

Mjini Brazzaville, chanzo cha serikali kimekanushaoperesheni yoyote ya vikosi vya usalama. Wakati huo huo, mazungumzo kati ya serikali na kambi ya Pasteur Ntoumi yameshindikana.

Mazungumzo kati ya serikali ya Congo na Ninja, wapiganaji wa zamani wa nchini humo yameshindikana. Pande zote mbili hazijafikia yoyote tangu miezi minne. Ujumbe unaomwakilisha Frederic Bintsamou, anayejulikana zaidi kwa jina la Mchungaji Ntumi, umekua unataka kuzungumzia siasa. Lakini ujumbe wa serikali, maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani, wametupilia mbali hoja hiyo. Ane Philippe Bibi, mmoja wa wajumbe wa Mchungaji Frédéric Bintsamou, amesema kuskitishwa na mwenendo wa wajumbe wa serikali: "Watu waliokuwa wakishiriki mazungumzo pamoja nasi hawakupewa majukumu na serikali ya kujadili masuala ya kisiasa. Waalipata majukumu pekee ya kujadili masuala ya usalama, hasa sula linalohusiana na Aprili 4, 2016 ".

Aprili 4, vikosi vya usalama vilikabiliana watu wenye silaha kusini mwa Brazzaville. Serikali inadai kuwa wapiganaji hao ni waasi wa zamani waliojulikana kwa jina la Ninja, wa Mchungaji Ntumi, ambaye alimuunga mkono mwezi uliopita wa Machi, Guy Brice Parfait Kolelas katika uchaguzi wa urais. Hao ndio serikali inataka kuzungumza nao, kwa mujibu wa msuluhishi wa mazungumzo, Paul-Marie Mpouelé.

Gari la Mchungaji Frederick Bintsamou, almaarufu Mchungaji Ntumi, ikiwasili katika eneo la Kisundi katika mji wa Brazzaville, Machi 17, 2016.
Gari la Mchungaji Frederick Bintsamou, almaarufu Mchungaji Ntumi, ikiwasili katika eneo la Kisundi katika mji wa Brazzaville, Machi 17, 2016. MARCO LONGARI / AFP

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.