Pata taarifa kuu
AFRIKA-DINI-UISLAM

Waislamu kusherehekea Idd-el-Hajj

Jumatatu hii Waislamu duniani kote wamesherehekea sikukuu ya Idd El Hajj wakiungana na wale (Mahujaji) walioko katika miji ya Makkah na Madina, nchini Saudi Arabia wakiendesha ibada mbalimbali.

Mahujaji wakizunguka Kaaba, kwenye Msikiti mkuubwa wa Makkah,Septemba 6, 2016.
Mahujaji wakizunguka Kaaba, kwenye Msikiti mkuubwa wa Makkah,Septemba 6, 2016. REUTERS/Ahmed Jadallah/File Photo
Matangazo ya kibiashara

Barani Afrika sikukuu hii imesherehekea katika nchi mbalimbali, huku baadhi ya nchi zikiwa katika hali ya sintofahamu kutokana na makundi yanayodai kuwa yenye msimamo mkali wa kidini, hasa nchini Somalia, Nigeria, Mali, Libya, Mauritania na nchi nyingine za Kiarabu barani Asia, na Ulaya.

Kati ya Waislamu duniani sikukuu hii hujulikana kwa majina mbalimbali ambayo hutafsiriwa pia kwa lugha mbalimbali kama vile:

Idd-al-Adhha yaani sikukuu ya sadaka
Idd-al-Qorban sikukuu ya sadaka (kwa kutumia neno tofauti ya "sadaka" katika Qurani); Kituruki: Kurban Bayramı; Kikurdi "Cejna Kûrbanê" ;
Idd-al-Kabir au "sikukuu kubwa"; "Bari Eid" huko Uhindi na Pakistan; jina hili hutumiwa kwa sababu kati ya sikukuu mbili zinazoamriwa katika Qurani hii ni sikukuu kubwa zaidi.

Sherehe huanza na sala ya idd katika Msikiti. Mara nyingi hufuatwa na baraza au mkutano wa Waislamu. Katika nchi nyingi huwa na kawaida kutembelea pia makaburi ya marehemu.

Kila Mwislamu mwenye uwezo hupaswa kumchinja mnyama wa sadaka siku hiyo mara nyingi kondoo lakini kuna pia sadaka za mbuzi, ng'ombe au ngamia kufuatana na uwezo na kawaida ya nchi.

Sehemu ya nyama ya sadaka hizo hugawiwa kwa maskini wasio na uwezo. Mengine hutumiwa kwa karamu ya familia

Idd husheherekewa kati ya tarehe 10 hadi 13 ya mwezi wa Dhul Hijjah wa kalenda ya Kiislamu. Tarehe hali halisi hutegemea na kuonekana kwa hilali au mwezi mwandamu. Hapa hutokea tofauti za kila mwaka kati ya Waislamu. Kimsingi mapokeo ya kiislamu hudai kuonekana kwa mwezi kwa macho.

Kubadilika kwa tarehe katika kalenda ya jua

Katika kalenda ya Gregori ambayo ni kalenda ya kawaida tarehe za Kiislamu hubadilika kila mara kwa sababu mwaka wa kiislamu hufuata kalenda ya mwezi lakini kalenda ya kawaida hufuata jua. Kalenda ya Kiislamu ni takriban siku 11 kasoro ya kalenda ya jua. Kila mwaka tarehe ya Idd huweza kutokea kwa siku mbili tofauti za kalenda ya Gregori kwa sababu kawaida ya Uislamu hufuata kuonekana kwa mwezi kunachopatikana tofauti duniani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.