Pata taarifa kuu
GABON-SIASA

Rais Ali Bongo atangazwa mshindi uchaguzi wa Gabon

Rais wa Gabon Ali Bongo ametangazwa mshindi wa Uchaguzi wa urais uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita.

Rais Ali Bongo wakati akipinga kura hivi karibuni
Rais Ali Bongo wakati akipinga kura hivi karibuni capitalfm.co.ke
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Mambo ya ndani wa nchi hiyo Pacome Moubelet-Boubeya Jumatano jioni alitangaza matokeo hayo ya mwisho na kubainisha kuwa rais Bongo alikuwa ameibuka mshinidi kwa kupata asilimia 49.80 ya kura dhidi ya mpinzani wake wa karibu Jean Ping aliyepata asilimia 48.23.

Ni ushindi mwembamba sana kwa rais Bongo ikiwa ni tofauti ya kura  5,594 kati ya watu 627,805 waliopiga kura katika uchaguzi huo.

Kabla ya matangazo hayo ya mwisho, Jumuiya ya Kimataifa ilitoa shinikizo kwa serikali na Tume ya Uchaguzi kutangaza matokeo ya mwisho.

Kikatiba, matokeo ya mwisho yalistahili kutangazwa siku ya Jumanne, ucheleweshwaji ambao ulizua hali ya wasiwasi.

Waangalizi wa Umoja wa Ulaya katika ripoti hiyo ya awali walisema kuwa, Uchaguzi huo haukuwa wazi.

Hali ya wasiwasi inashuhudiwa nchini humo, na kumeripotiwa makabiliano makali kati ya wafuasi wa Jean Ping katika jiji kuu la Libreville, aliyekuwa amejitangaza mshindi.

Mwaka 2009 vurugu zilizuka baada ya kutangazwa kwa matokeo ya mwisho.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.